Mkakati wa Njia Tatu Kukimbia Tamaa



Lakini zikimbie tama za ujanani; ukafuate haki. na imani. na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi. 2 Timotheo 2: 22

Andiko hili ni moja ya maandiko yaliyojaza ujumbe wa ushauri jinsi tunavyoweza kushinda tamaa. Ni hekima kukariri maandiko haya na kuyaweka moyoni. Yatafune haya kila siku. Ruhusu akili yako inywe andiko hili.

 Kimbia Kutoka…. “Lakini zikimbie tama za ujanani;”

“Tamaa” ni matamanio, nia au hamu zetu. Lakini hasa andiko hili linazungumzia “tama za ujanani”. Na tamaa hizi za mwili zinaelezwa “ kufanya vita dhidi ya nafsi zetu” (1 Petro 2:11). Kwa nje matamanio haya yamefungwa kwenye viungo vya miili yetu (Warumi 6:12),lakini tukiangalia ndani tunaona shina lake ni katika moyo wenye dhambi (Warumi 7:7). Na hatimaye tamaa hizi zinadhihirika katika ibada za sanamu (Kolosai 3:5), zikiyafanya maisha na tamaa zetu zitupeleke kutumikia viumbe badala ya Mungu Mwumbaji.

Kila Mkristo, hata kama amejazwa sana na Roho wa Kristo, bado anaishi katika mwili wa kufa unaozungukwa na burudani za kidunia. Tamaa hizi za ujanani siku zote zipokaribu nasi zinatufuata. (Mwanzo 4: 5-7). Kila tunapoziona zinaibuka ndani yetu lazima kukimbia. Kukimbia hivi:

1) Kiakili: kuepuka kutafakari mambo maovu

2) Kwa kuona: kuepuka kutazama mambo /picha zenye kuamsha tamaa. 

3) Kimwili: kuondoka (kwa miguu) katika mazingira yenye kuamsha tamaa 

Kimbilia Kwa .. “….. ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani,” 

Haitoshi tu kukimbia tammaa za ujanani. Lazima tukimbie kuelekea matamanio mengine. Lazima tukimbie kuelekea kumfanana Kristo. . Kristo ameahidi watu wake moyo wa: 
1) Haki (uadilifu wa kweli, nia ya kutenda haki, na maisha ya kumpendeza Mungu)

2)Imani (ushawishi wa ndani wenye uhakika katika kumwamini Mungu)

3)Upendo (moyo wa ukarimu kwa Mungu na kwa watu wengine) 

4)Amani (utulivu moyoni na maelewano mazuri na Mungu na watu wengine) .


Tunahitaji kuyakimbilia kwa bidii mambo haya tukijua kwamba ndivyo tulivyoumbwa tuwe. Tuyakimbilie tukijua haya ndiyo hatima yetu. Kwa maana baada ya maisha haya tutakuwa tukiishi maisha ya haki, na imani, na upendo, na amani, katika ufalme wa Mungu. Tukiishi kwa matumaini haya tunajitakasa. (1Yohana3:3).

Kimbia Na ….. “……pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi”.

Hatutakiwi tu kuzikimbia tamaa na kuyaelekea maono ya Mungu juu ya maisha yetu tu, bali tunapaswa kukimbia pamoja na ndugu zetu wenye maono sawa na sisi, wale wenye imani, msimamo, na mapambano kuelekea utakatifu kama sisi.

Marafiki hawa lazima wawe wale wanao “liitia jina la Bwana”, yaani watu waliookoka (Mdo 22:16; Warumi 10:13). (Yakobo 5:16). (Waebrania 10:24-25).

KUKIMBIA KUNAHUSISHA YAFUATAYO:

1. EPUKA kwa kadiri uwezavyo na ilivyo sahihi mazingira yanayoweza kuamusha tamaa (2 Timotheo 2:22). “Make no provision for the flesh, to gratify its desires” (Warumi 13:14).

2. Sema HAPANA dhidi ya tamaa kila sekunde tano. Sema kwa mamlaka ya Yesu “ kwa jina la Yesu hapana”. ( Yakoba 4:7). Uwe mwua dhambi vinginevyo itakuua

3. GEUZA ufahamu wako kuelekea kwa Kristo ambako ndiko kwenye utoshelevu mkuu. Kusema tu hapana haitoshi, lazima kuweko mbadala (Waefeso 4:22). (1 Petro 1:14). (Mithali 7:22). Ujinga hushindwa na elimu, giza na nuru, uongo na ukweli. Hivyo baada ya kusema hapana lazima kumtafuta mwenye ukweli.

4. SHIKILIA ahadi za Mungu na uwe na matumaini/usibabaike. (Waebrania 3:1). (Mathayo11:12). 5. BURUDIKA na mambo ya Mungu (Zaburi90:14-17). 6. ONDOKA kwenye Mazingira hatarishi, na jiingize kufanya kazi za maana (Warumi12:11). (1 Wakorintho 15:58). (Tito2:14).

Maoni

  1. Be blessed kwa hiki chakula.. Na kikakae ndani ya moyo wangu na kikaishi..

    JibuFuta
  2. Amen, Mungu aendelee kukufunulia zaidi

    JibuFuta

Chapisha Maoni