NGUVU YA KUZALIWA-KUNA MAMBO UNGEYAJUA UNGEGOMA KUZALIWA
Jesus, nilitaka nianze kucheka wakati naanza kuandika hiki chakula cha nafsi maana inachekesha kwa ndani kidogo. Ndio, kama umekuwa unafuatilia mfululizo wa somo hili la NGUVU YA KUZALIWA basi utakuwa unaendelea kufichuka toka katika kila eneo ambalonimeandika huko nyuma. Kimsingi, somo hili ndio namna yangu ya kufundisha na kuelezea KIFURUSHI CHA KUSUDI LA MUNGU KWAKO kwa namna ambayo unaweza kuielewa bila kulazimisha. Kwa hiyo unaposoma elewa kuwa unajivumbua na kulivumbua shauri la Mungu kwako katika kizazi chako. Pia ndio njia ya kujua thamani na umuhimu wako hapa duniani. Kutambua maono yako na kwanini uko jinsi ulivyo. Kwa hiyo unapoendelea kusoma elewa kuwa ilibidi tu uzaliwe maana ulishapangiwa kazi na ukapewa na mtaji ndani ya kifurushi cha kuzaliwa kwako. Haya tuendelee sasa.
Fikiria Mungu angekwambia, kabla hajaruhusu mimba yako itungwe tumboni mwa mama yako, angekuonyesha kila kitu ambacho ungepitia na kingekupata toka kuzaliwa mpaka namna ambavyo ungekufa ungekubali? Fikiria uliyopitia mpaka sasa, na huenda hata sasa tu bado kuna mambo lukuki huyaelewi na unatamani hata kufa, sasa haya ulopitia mpaka sasa ndo ungeyajua ukiwa katika WAZO LA MUNGU ungekubali kuja duniani? Yaani kaa ufikiri kwa makini, ungejua ungezaliwa na wazazi kama hao waliokuzaa, wasio na elimu, wenye elimu lakini wako kama sanamu za kuchongwa, masikini na wanaoishi maisha ya viraka ungewakubali kweli? ungekubali kuishi maisha ya kimasikini mpaka uje upate kazi ili wewe ndo uwe ufunguo wa mafanikio kwenu? Ungekubali kama ungejua mapema kuwa utapata mimba kadhaa na zote utatoa na utakufa ukitoa mimba ya tisa? Ungeona ile ajali iliyokukata miguu ukabaki kilema lakini bado unaishi ungesema uko tayari kuja duniani?
Tuwe wakweli, nani angependa kuzaliwa nchi kama Tanzania kama ungepewa nafasi ya kuonyeshwa nchi zote dunaiani? Ungekubali kuzaliwa kwenye kabila kama hilo kweli? Kabila linasifika kwa uchawi, kabila linasifika kwa kupenda pesa, kabila linasifika kwa majivuno na kiburi, kabila linasifika kwa kuongea kama chiriku, kabila linasifika kwa kupenda ngono, kabila linasifika kwa ukali na ubabe, kabila linasifika kwa kuombaomba, kabila linasifika kwa umbea na majungu, kweli ungekubali kwa moyo wa dhati kuwa sehemu yake?
Ungeonyeshwa jinsi utakavyoishia darasa la nne, na ukaanza kuhenya kufanya biashara ambayo ingefanikiwa ukiwa na miaka 50 ungekubali? Nani anapenda mahangaiko? Kwani unadhani Mungu alikuwa hajui kuwa utakataliwa na wazazi wako? Wewe kaa chini ufikirie tu kuwa baba yako atakukataa ukizaliwa, na mama yako atakutupa chooni halafu majirani watasikia kilio cha mtoto na waje kukutoa umepakwa kinyesi, ungekubali kuzaliwa na hasa na hao wazazi? Jiangalie wewe mama yako kapata mimba na unaona anenda kwa daktari kukutoa na unakuflash chooni? Ungekuwa ni wewe unaweza kuona hayo mambo ungekubali? Nataka utafakari vizuri maana huenda bado umejaa malalamishi, unawalaumu wazazi, umeshamlaumu sana Mungu, shetani ndo kabisa ingawa ambaye bado hujamlumu ni wewe mwenyewe. Nataka utafakari juu yangu nguvu ulonayo ya kubadilisha chochote katika historia ya mambo ambayo yamekutokea mpaka sasa na yanakufanya ukate tamaa.
Hujajua nguvu ya kuzaliwa? Wewe haya machache tu yanakutaabisha kwa kiwango ambacho unatamani kufa, sasa hebu fikiria moyo wa Mungu ni mkubwa kwa kiwango gani, kwani aliyajua hayo yote nab ado akaruhusu uzaliwe. Ndio, alijua kuwa wewe utakuja kusumbua sana mtaani, alijua utakuja kubwia unga, alijua utatoa mimba, alijua utalawitiwam alijua utakuwa shoga, alijua utakuwa msagaji, alijua utalawiti wengine, alijua utakuwa tapeli, alijua utakuja kuvaa chupi ukaiita kimini, alijua kuwa utafanya mambo nje ya wakati na kupata matatizo, alijua yote usiyiyajua na machache unayoyajua sasa. Pamoja na mengi hayo yote bado akaruhusu uzaliwe kwakuwa kusudi na ile nguvu. Nguvu ya kuzaliwa ni kusudi la maisha yako ambalo ni KIRUFUSHI chenye mambo mengi sana.
Ungejua yote ambayo mpaka sasa yalikukatisha hata tamaa, ungejua yote yaliyokufanya usione tena thamani ya maisha, ungejua yote ambayo ungekosea na kujisababishia majanga katika maisha yako nay a wengine, ungejua utakuja kupata magonjwa ya ajabu kwasababu ya dhambi na ujinga wako, ungejua kuwa utaitwa Tabu au Masimango au Sikitu au Shida au Matatizo na yote hayo ungeyaona kwa mbali ungekubali hilo jina? Ni vizuri ukajiuliza kwa kina ili upate sababu kubwa zaidi ya kumkubali Mungu aliyejua hayo yote na bado akawa pamoja na wewe. Ili upate sababu kubwa zaidi ya kumshukuru Mungu kuliko kudhani ilikuwa bahati mbaya ajali au sijui nini yaani.
Ingekuwa kuzaliwa kwako ni ajali ingewezekanaje uzaliwe baada ya miezi tisa? Kwanini usingezaliwa siku umetungwa mimba? Kwanini usingezaliwa ukiwa na miezi mitatu? Kwanini? Ingekuwa ni ajali kwanini mambo yametokea kwa mpangilio ambao umekufiksiha kwenye eneo ambao unaanza kuelewa kuwa Mungu ana nguvu kuliko wewe? Ungekimbia mpaka wapi kwa mfano ili usizaliwe? Ulikuwa na uwezo gani wa kuzuia kuzaliwa kwako? Aliyekujua alipanga na kukusudia wewe uzaliwe pamoja na magumu yote ambayo ungepitia. Kwani, wewe t undo una matatizo dunia nzima? Wewe ndo wa kwanza? Au ndo wa mwisho? Ni wa pekee sana wewe kiasi ambacho unaona hujatendewa haki kabisa kwa kufanyiwa mambo ulofanyiwa. Unataka upige kelele kwamba umebakwa kwenye nyumba ya wageni?
Acha jambo hili likuingie akilini leo. Hata Bwana Yesu nae alikutana na mengi na kibaya zaidi alitakiwa kufa kwa dhambi amabazo hajafanya. Alishawahi kusahauliwa na wazazi wake mjini. Alishawahi kukataliwa na marafiki zake karibu. Alishawahi kusalitiwa na mtunza fedha wake. Alishawahi kuonekana ana wazimu na ni kichaa na ndugu zake. Alishawahi kulia. Alishawahi kuumia. Alishawahi kumuomba Mungu amuepushie mateso yaliyokuwa mbele yake lakini ikashindikana. Aliona aibu mbele yake, aliona Pilato atanawa maji na kujifanya hana hatia. Aliona ile misumari. Akaona ule msalaba. Akaona atakavyodhalilishwa na kubakizwa uchi. Aliona ile kiu pale msalabani. Aliona mkuki ubavuni. Aliona watu aliokuja kuwasaidia wakimdhihaki na kumzomea. Aliona yule mwizi pale msalabani akimdhihaki pia. Aliona wale askari wakipigia kura nguo yake. Aliona akifa na kuitoa roho yake. Aliona akishuka kupambana na shetani. Angegairi ingekuwaje kwako leo? Je, ulishasoma popote kwamba alishawahi kulalamika kuwa Mungu anamuonea?
Tafakari vizuri. Ndo maana nilianza kukwambia kuwa kuna mambo ungeyajua kabla hujazaliwa usingekubali kuzaliwa maana moyo wako ni mdogo kama mbengu ya mchicha. Sasa, umeona uhalisia, Mungu ana kusudi na maisha yako. Kwanini leo usifanye maamuzi makubwa na mazuri na sahihi? Jiachie kwa Mungu. Jikabidhi na umuombe akusaidia kusimamia lile kusudi alilokuumbia. Ndio, ipo sababu kwanini ilikuwa wewe uzaliwe na sio mwingine. Ipo sababu. Ni Mungu tu ndo anaweza kukujuza. Hebu tafakari mambo mazuri ulofanya mpaka sasa. Dunia ingekuwaje bila wewe? Si unaona ilikuwa ni lazima tu uzaliwe kwa mapenzi ya Mungu.
Sasa tumia kila ulichonacho kumtukuza Mungu kwani hakuna ambacho ni mali yako. Hukuzaliwa umevaa viatu au umevaa saa au umeshika simu mkononi. Hukuja na kitu zaidi ya mwili ulio uchi. Mungu alijua namna utakavyoishi. Alijua utazaliwa na nani. Alijua utazaliwaje. Alijua utazaliwa lini. Alijua utazaliwa ukoo gani. Alijua utazaliwa wapi. Alijua utazaliwa ukiwa kinjiti au bonge. Alijua. Huwezi ukamshangaza Mungu kwa kumsimulia hayo yote maana yeye ndo mwandishi stadi wa maisha yako. Wajibu wako wewe ni kujua na kutembea katika KURASA ZA MAISHA YAKO.
Raphael Joachim Lyela
YKM Founder
Amen.. Nimebarikiwa.
JibuFutaBe blessed Dad
Aisee hyo iko pouwaa sana Dad....inatufundisha sana kutembea katika malengo ya maisha yetu.
JibuFutasijui nilikuwa wapi siku zote, basi tu yani. Kuna vitu mpaka huwa najiuliza kwanini visifundishwe labda hata kwenye tv station kubwa duniani. Kama mataifa wanaweza kutumia tv kurusha vitu ambavyo ni meaningless kwa jamii, yani unakuta kwa mfano,mashoga wananunua vipindi kwenye redio au tv kubwa na kutangaza ujinga na upuuzi wao na jamii inaiga na hata kuathiri pia,au watu wanaonyesha vichupi na utupu kwa pazia la fashion show. Hivi haiwezekani kweli kwa vitu vizuri kama hv vihubiriwe duniani?. Sijui tu yani,ngoja niishie kwa hapa.
JibuFuta