Pakua Uwezo:Huwezi kusema umezaliwa bila nguvu ndani yako, yaani uwezo wa kusababisha na kuleta mabadiliko kwako na kwa jamii kubwa kuliko wewe,yaani kizazi chako na kizazi kijacho.Mungu hajawahi kuumba MTU ASIYE NA THAMANI,kuzaliwa tu kwenyewe ni ishara kwamba umeruhusiwa kuja kudhihirisha kuwa MUNGU HAKOSEI. Changamoto moja tu unatakiwa uishinde,GUNDUA NINI KINAFICHA UWEZO WAKO. Kumbuka bila kujua uwezo wako unafichwa na nini ni vigumu sana KUPAKUA. Sasa kama ni dhambi ndo inaficha basi tubu leo, kama ni uoga basi acha leo, kama ni historia mbaya basi samehe leo...HUWEZI KUPAKUA USICHOKUWA NACHO..uzuri ni kwamba HAKUNA ASIYE NA KITU. Pakua Uwezo wako, acha kutubania.
Mgodi Fichuka na Raphael JL:
Maoni
Chapisha Maoni