Sababu 43 za mimi kuziepuka picha za ngono.

1. Uhusiano wa upendo anaonionesha Bwana Yesu unanipa raha zaidi kuliko picha za ngono.

2. Naepuka picha za ngono ili nikamilishe utambulisho wangu kama mtoto wa Mungu.

3. Sijihusishi kuangalia picha za ngono kwa sababu neema ya Kristo katika maisha yangu inaniwezesha.

4. Siangalii picha za ngono kwa sababu ninaufurahia ujazo wa uhuru wangu katika Kristo Yesu.

5. Siangalii picha za ngono kwa sababu ninaepuka maisha ya udanganyifu yaani kudanganya kihisia kwa picha za ngono.

6. Siangalii picha za ngono kwa sababu ninajijengea ufahamu makini wenye hisia za Kimungu.

7. Ninaepuka picha za ngono ili nisijiingize kwenye mtandao wa kupenda makahaba.

8. Ninaepuka picha za ngono ili kujiepusha na tamaa ya ibada ya sanamu iliyo katika picha za ngono.

9. Ninaepuka picha za ngono ili niwe wakili mwaminifu wa pesa yangu, maana kutoa pesa kununua MB za kuingia kwenye mtandao niangalie picha za ngono ni kukosa nidhamu na uaminifu katika pesa.

10. Ninaepuka picha za ngono ili niwe wakili mwaminifu katika muda wangu. Sitaki kupoteza muda kwenye kuangalia uchafu wa ngono.

11. Ninaepuka picha za ngono ili nijiepushe na kuziwezesha kampuni zinazotengeneza picha za ngono maana wanapata pato kubwa kwa watu kuangalia picha hizo. Ni bora nikawezesha kazi ya Mungu kusonga mbele.

12. Ninaepuka picha za ngono ili nitunze uthamani wa zawadi ya tendo la ndoa alilokusudia Mungu kwa wanadamu.

13. Ninaepuka picha za ngono ili nilinde usafi wangu na nguvu ya kifikra aliyonipa Mungu.

14. Ninaepuka picha za ngono ili nikue katika tabia njema.

15. Ninaepuka picha za ngono ili nilinde heshima ya ushuhuda wangu kama Mkristo.

16. Ninaepuka picha za ngono ili niidumishe afya yangu ya kiroho na ushirika wangu katika mwili wa Kristo.

17. Ninaepuka picha za ngono ili nijijengee uwezo mkubwa wa kupinga mahusiano ya kimapenzi nje ya mapenzi ya Mungu.

18. Ninaepuka picha za ngono ili niweze kulea mtazamo sahihi na wa utakatifu wa kibiblia katika jinsi inavyonipasa kuangalia uwanauke.

19. Ninaepuka picha za ngono kwa sababu ninamchukulia mwanamke sawa na mimi na ni wa thamani.

20. Ninaepuka picha za ngono ili nijifunze kuishi kiuhalisia na sio maisha ya kufurahia kitu ambacho hakipo halisi.

21. Ninaepuka picha za ngono ili nisiwe na maisha ya hukumu moyoni pamoja na aibu.

22. Ninaepuka picha za ngono ili nijitengenezee maisha ya utoshelevu na kuridhika katika ndoa. Mtu anayeangalia picha ngono hawezi kuridhika wala kutosheka na mwenzi wake.

23. Ninaepuka picha za ngono kwa sababu ninaishi maisha ya baraka utumishi wangu kwa Mungu na uaminifu.

24. Ninaepuka picha za ngono ili nijifunze mbinu za kimahusiano katika maisha ya ndoa.

25. Ninaepuka picha za ngono ili kujiepusha na makovu ya baadaye ya kiroho, ya kiuufahamu na ya kihisia.

26. Ninaepuka picha za ngono kwa kuwa ninayaishi maisha ya furaha katika Kristo Yesu.

27. Ninaepuka picha za ngono ili nipate thawabu ya milele.

28. Ninaepuka picha za ngono kwa kuwa ninajifunza kushughulika na vyanzo vya matatizo yangu kuliko kutibu matatizo yenyewe.

29. Ninaepuka picha za ngono ili kujikinga kuwatamani wengine katika nafasi niliyonayo.

30. Ninaepuka picha za ngono kwa sababu ninaheshimu nguvu kubwa waliyowekeza wale walionilea kiroho.

Kama ni mwana ndoa:

31. Ninaepuka picha za ngono kwa sababu ninajiepusha na uzinzi katika moyo wangu.

32. Ninaepuka picha za ngono kwa sababu ninautia moyo uaminifu wa mke wangu kwangu.

33. Ninaepuka picha za ngono kwasababu ninaheshimu agano na nadhiri zangu za ndoa na uaminifu.

34. Ninaepuka picha za ngono kwa sababu ninatunza uhusiano wa ndoa mbali na hisia za uongo kwa wanawakae walio katika filamu za ngono.

35. Ninaepuka picha za ngono kwa kuwa ninamuheshimu mke wangu.

36. Ninaepuka picha za ngono ili kujiepusha na kufungua mlango wa mambo ya zinaa.

Kama nina watoto:

37. Ninaepuka picha za ngono kwa sababu ninapunguza hatari ya watoto wangu kujihusisha na mtego huo wa picha za ngono.

38. Ninaepuka picha za ngono kwa sababu nataka kuwa mfano wa maadili mema kwa watoto wangu.

39. Ninaepuka picha za ngono kwani ninakwepa kuaibika na kuwaaibisha watoto wangu.

40. Ninaepuka picha za ngono kwa kuwa nataka kuwatia moyo wote walio na mtazamo chanya katika maisha yao.

41. Ninaepuka picha za ngono ili kuwatia moyo wote wanaoniamini katika utumishi wangu.

42. Ninaepuka picha ya ngono kwa sababu nitaijenga roho ya uzinzi katika maisha yangu.

43. Ninaepuka picha za ngono kwa sababu hazina faida katika maisha yangu ya kiroho na kimwili.

Kwa ushauri wasiliana na  Dr. Gunewe

Maoni

  1. picha za ngono zipigwe vita katika mitandao

    JibuFuta

Chapisha Maoni