TAREHE KAMA YA LEO 23/09/2012 YKM (YOUTH KINGDOM MINISTRIES) ILIZALIWA.
FOUNDER WA HUDUMA HII NI PASTOR RAPHAEL JOACHIM LYELA.
HIVYO LEO TUNAADHIMISHA MIAKA MINNE YA UWEPO WA HUDUMA HII.
YKM ni kifupi cha
Youth Kingdom Ministries.
Huitwa Ministries kwa
sababu ndani yake kuna huduma (Ministries) tisa.
YKM ni huduma
ya vijana na inaendeshwa na vijana. Huduma hii haifadhiliwi na mtu yeyote zaidi
ya members wake wenyewe.
Huduma hii haipo
chini ya dhehebu lolote bali ipo na inatumikia ufalme wa Mungu.
Mwanzilishi wa huduma
hii anaitwa Raphael Lyela na anakaa Dodoma kwa sasa. Wengi wetu humwita daddy!
KUSUDI LA KUWEPO YKM
“Kuwafanya vijana
kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo kwa kuwafundisha Neno la Mungu ili wapate ufahamu
sahihi utakaowasaidia katika maisha yao ya sasa na ya baadae kwa ajili ya
utukufu wa Mungu na Ufalme wake”
MAONO YA YKM
“Kuwa chombo
kinachoaminika kwa kuwafikia na kubadilisha mfumo wa fikra wa vijana ili uwe
sawa na Neno la Ufalme wa Mungu kwa ajili ya kuleta mabadiliko na matokeo
katika familia, jamii na taifa kwa ujumla na kwa utukufu wa Mungu ”
HUDUMA ZA YKM
1.Mindset
Upgrade:(Empowered for transformation,Romans 12:1-2). Uhusika na kubadilisha
mtizamo wa vijana kwa kutumia neno la Mungu.
2.Kingdom
Transformers: (Leadership that transforms,Acts 17:6) Uhusika na kuandaa
viongozi katika Nyanja mbali mbali za maisha.
3.The Bridge is
Today:(Shaping your destiny today,Proverbs 12:1).
Uhusika na kukutoa
katika ulicho fanya zamani na kukuonesha waweza fanya nini ili uwe na
future nzuri.
4. Kingdom
Worship:
(His presence,my
destiny;John 4:23) Uhusika na kutuongoza kumwabudu Mungu kwa usahihi.
5. Kingdom
Charity:
(Impacting through
giving;Acts 20:35)
Uhusika na kuwafikia
wahitaji.
6. Kingdom
Ladies:(Ladies with value,Ezra 9:2):Uhusika na kuandaa wadada watambue thamani
yao.
7.Gospel Corner:
(Youth to Jesus.Youth
in Jesus.Youth in Jesus, Mathew 28:16-20).
Uhusika na kuwafikia
watu na injili ya wokovu.
8.Kingdom Gents:
(Performance1Kings
2:2-3, Col 1:14 & Psalm 125):Uhusika na kuandaa wanaume watakao yatambua na
kuyasimamia majukumu yao ya kiume.
9. Kingdom
Inspiration:
(Inspired for
influencing generations, Isaiah 41:6-7): Uhusika na kuinua mioyo ya
watu kwa kuwatia moyo kwa misingi ya neno la Mungu.
Huduma hizi zote zina
viongozi
YKM MIKOANI
YKM inafikia mikoa
ifuatayo mikoa ifuatayo kwa sasa:
Ruvuma, Dar, Arusha,
Mwanza, Iringa,Mbeya, Kilimanjaro, Dodoma ,Morogoro na tunazidi kuelekea kwenye
mikoa mingine kadri siku zinavyoendelea.
Kila mkoa una uongozi
wake wa viongozi Kumi.
UTENDAJI WA YKM
YKM inawafikia vijana
na mafundisho kwa njia ya:
1. Simu zao ( SMS na
Whatsapp)
2. Kwa njia ya
mtandao Tovuti na Facebook
(http://www.ykmjesusup.org/
and https://www.facebook.com/YouthKingdomMinistriesJesusUp )
3. Kwa njia ya
Events mikoani mwao.
Mikoa iliyotajwa hapo
juu ina whatsapp grups unaeza unganishwa kama upo whatsapp.
Kwa taarifa zaidi
tembelea tovuti yetu: http://www.ykmjesusup.org/
MAJUKUMU YA MWANA YKM
Members wa YKM
wanamajukumu yafuatayo.
1.Kusambaza message
za YKM ili habari njema iwafikie watu wengi zaidi.
2.Kushirikiana na
members wenzako kuipeleka injili ya Kristo kwa kipaji chako na hata mali zako.
MANUFAA YA YKM KWAKO
Utapata manufaa
yafuatayo:
1. Utakua kiroho
2. Utapata
platform ya kumtumikia Mungu
3. Utapata
familia kubwa sana ya vijana wenzako watakao kupenda na kukujali kwa dhati
4. Utakua pia katika
Nyanja nyingine za kibinadamu (holistic human development)
5. Nk.
This is a brief about
YKM, utazidi kuifahamu huduma kadri utakavyo jihusisha nayo.
Maoni
Chapisha Maoni