By
Raphael JL:
Kwenye mahusiano,kama nilivyosema kwenye somo lililopita,
yako mengi yanayochosha sana na hasa kama haujasimama na Mungu na kuwa na
utulivu wa ndani wa kusikia na kumsikiliza Mungu anavyosema na kukuongoza
kupitia mawazo,fikra na hisia zako kufanya uchaguzi wa mke au mume ajae.
Nilisema kwenye somo la nyuma kuwa haijalishi mmekutana wapi au mtumishi gani
KAKUPIGIA PANDE,lisije likawa pande la msumari kooni, ila sasa nataka niendelee
na sehemu ya pili na kubwa sana,kaa mkao wa kujifunza.
UNA UHAKIKA? Je, ukiulizwa leo, kama una uhakika na mtu
uliye naye utasemaje? SIO LAZIMA UKOSEE KOSA LA BABA YAKO KAMA ISAKA NA
YAKOBO,ila unaweza kuchagua mwenyewe kutegemeana na hali unayokuwa nayo.
Umekutana na mtu kwenye gari,au kwenye huduma, au kwenye mamtatizo au alikuwepo
akikutia moyo wakati umefiwa na wazazi na mwisho mkajikuta mko connected...ni
kweli kuwa something has to connect you to someone...whatever connect you to
someone will sustain you or break you...sasa hapo ndo tupaangalie leo na kuona
nafasi ya ROHO MTAKATIFU...kwenye mahusiano hayo hayo...hii ni kuepuka maumivu
ya makusudi na kujitakia...kumbuka SUKARI HAIWI CHUMVI KWA KUICHANGANYA NDANI
YA ASALI....
KIWANGO CHAKO CHA KUMJUA:Roho Mtakatifu hasemi uongo wala
hadanganyi ila sisi tunajua yeye ni msaada wetu, mshauri wetu na pia mwalimu
wetu.Wote waliomtegemea hawajajuta.Mfano, mkaka kamfuata mdada na gear ya BWANA
KASEMA,mdada kwakuwa alikuwa anasubiria sana hiyo nafasi anakubali kwa sauti
ambayo hajaisikia yeye mwenyewe,anamwaga moyo wake na kuamini yaani kama Bwana
kasema itakuwa lazima niwe hivo tu...so wadada wengi wamejikuta wanaingia
KICHAKANI kwa kudhani hivo tu yatosha...fahamu kuwa kichaka kina vitu vingi
sana ambavyo usingependa kuviona au kuvijua....
DONT ABORT THE PROCESS:Roho Mtakatifu yupo na anatusaidia
mengi tu, nakubali kuwa Mungu anaweza kuzungumza kwa njia yoyote ile na hata
sasa najua anasema, na najua yapo mahusiano ambayo kabisa Bwana alisema na
ikawa ndo kasema hivo moja kwa moja...lakini kwasababu ya kutokumjua na
kumsikiliza ROHO WA MUNGU vijana wengi wamekuwa WANAHARIBU MCHAKAKATO...ni
hatari sana kujikuta umeolewa na mkwe wako na sio rafiki yako...kumbuka urafiki
unatengenezwa.....sasa ndo nasema hivi hapo....USIHARIBU MCHAKATO....hata kama
Bwana kasema inabidi umuulize kama ndo kakwambia uende ukamwambie muhusika
kwani kwa kukurupuka kwako unaweza ukajikuta UMEHARIBU MCHAKATO.....friendship
is a function of social UNGAPPING...so ukianza na ishu zako za kiroho from
point A unaweza ukajikuta umoa au umeolea na kitu ulichokuwa unakiogopa kwa
miaka mingi...ni hatari sana....
WASAIDIZI WA ROHO MTAKATIFU: Walipowaona mnaimba pamoja,
mnakula pamoja, mnatembea pamoja, mna huduma inayofanana, mna sura
zinazofanana, mnatokea mkoa mmoja na hata mna kabila moja...basi wakaibuka
manbii 400 wa BAALI ambao wakaanza kuwafananisha na kuona nyie mnafanana hakika
na inawapasa kuoana...na nyie kwa KUJAA MAJI mnaanza kutengeneza mazingira ya
KUUTIMIZA UNABII WA MFALME KORESH,laiti kama ungejua kuwa MAISHA YA NDOA ni ya
watu wawili na Bwana Yesu katikati...mkishaona mtagundua haha hahaha heee KUMBE
HATA HAMFANANI...umeoa mke wa mtu mwingine...umeolewa na mume wa mtu mwingine...umelazimisha.....NAFASI
YA ROHO WA MUNGU HAPO IKO WAPI? Sikatai kuwa Mungu anaweza kuwatumia watu
kutukutanisha na watu wetu sahihi...ila USAHIHI WA HAO WATU TUNAUPATA WAPI? NI
HATARI SANA KUUTEGEMEA UPEPO.
Kama humuamini Roho Mtakatifu basi hilo ni tatizo la kipekee
sana,maana utaendelea kutibu vidonda mpaka uchakae...kimsingi Roho wa Bwana
yupo na anafanya kazi....sema kuna wajinga fulani wamekuwa wanatumia vibaya na
kumsingiziia na kumbe ni hisiaa zao from ISIDINGO...na ndo maana mwisho wa siku
inaonekana kama Roho Mtakatifu hayupo na hafanyi kazi lakini kimsingi ni
UKIROHO WA WAROHO WACHACHE tuuuuu...
Ndio...yaani unaoa na kuolewa na mtu wa kulazimisha au
kudanganywa na kisha unaingia nae ndani na unaona kama vile unaishi na
mkweo...yaani huna uhuru...yaani huna amani na unaona kabisa...yaani
unashuhudiwa kuwa ulichemka kabisaaaaaaa na unaiona waziwazi....unatamani ufe
na hufi...unatamani na kuomba afe na hafai MPAKA MMELIPA GHARAMA YA KUHARIBU
MCHAKATO...hapo ni kama umeoa mkwe vile...utatamani uchelewe kurudi home ili
ukute amelala....vyvote itakavyokuwa yaaani ila utajiona tu ni kama UMEVAA NGUO
ZA JESHI NA UNAENDA KUOGELEA....
VITISHO VYA KIVULI USIKU: Mungu yupo na anaweza kukusaidia
kuvuka hakika, ila sasa unajikuta unakosea maana una haraka ya kuolewa au kuoa
maana unaona umri unaenda, unajiona umeanza kuwa mzeee fulani hivi, unajiona
mwili wako unaanza kupoteza mvuto wa kisichana, unajiona unajinenepea tu na
hupendi, unajiona tu unahamu sana ya kuwahi KUOLEWA NA KUOA na mwisho kumbe
ulikuwa unawahi KWENYE SHAMBA LA MBIGIRI NA UKO PEKU...WENGINE WANATAKA WAWAHI
KUOLEWA na kuoa ili wazae mapema...haha hahah hah kazi kweli...so mwisho wa
siku wanaoelwa na kuoa halafu wanagundua hawazai maana UWEZO WA KUPATA MTOTO
hauko kwenye haraka za kuoa na kuolewa..ila sasa unafanye...na ikitokea umezaa
basi unawafanya watoto wako kuwa wapenzi wako kwani hupati UNACHOSTAHILI, yaani
unapata ULICHOTAKA ambacho ni watoto...ni hatari sana KUKIMBILIA
USIKOJUA...UTAJIKUTA UMEKUMBATIWA NA MTU KAVAA KOTI LA UPUPU....
Maoni
Chapisha Maoni