TAFAKARI YA SIKU- JUMANNE



Ambassador of Christ
YESU Asifiwe..

Kumbuka hili siku zote

"Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa KRISTO"  2Kor 11:3

FIKRA ziliumbwa zikae ndani ya nafsi ili zitumike kuweka aina na kiwango cha maisha ya katika eneo linalomuhusu. Ndani ya nafsi kuna FIKRA na Biblia inatufundisha nini kipitia mstari wa Wakoritho:, ni kwamba shetani akitaka kumvuruga na kumwaribu mtu moja kwa moja uenda kuvuruga FIKRA zake maana ndani ya FIKRA ndiko kwenye chemchem ya kutimiza kusudi na ndiko kwenye maarifa ya kukufanya ustawi na kufanikiwa. Jiulize swali hili pamoja na mimi..kama una simu yenye uwezo wa ku install all social media na pia ina uwezo wa ku install Bible Application ni mara ngapi kwa siku ufungua simu yako kusoma hata mstari mmoja wa Biblia? Na ni mara ngapi kwa siku utumia simu hiyohiyo kusoma mambo yaendayo na yatukeayo kupitia social media's na wakati mwingine si hata ya muhimu? Kwa nini uzito uwe kwenye kusoma Bible na ninayo kwenye simu? FIKRA zangu kwenye kusoma msgs zenye ujumbe wa KIFALME na kusoma msgs za story nazitumiaje? Sisemi social media ni mbaya au Simu ni mbaya ila nasema FIKRA zangu nazitumiaje kujenga UFALME? FIKRA zangu nazitumiaje kwenye matumizi ya simu na Internet? Mangapi ya muhimu yanipayo maarifa nayasoma na kuyapitia kwa siku kwa kutumia simu yangu? Tamani kuona FIKRA mpya kwako achilia DAMU ya YESU kwenye kila ufanyalo!

UFALME KWANZA

Naibariki wiki yako
Naibariki Jumanne yako

..."Jesus Up"...

Maoni