TAFAKARI YA SIKU- JUMATANO


Ambassador of Christ
YESU Asifiwe..

Kumbuka hili siku zote rafiki

"Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote wala usizitegemee akili zako mwenyewe" Mith 3:5

Biblia haikusema uzisitumie bali usizitegemee tena pale zinapotumika zenyewe!

MUNGU alipotuumba alitupulizia pumzi hai, alitupulizia pumzi yake na ndani ya hyo pumzi kulikuwa na nafsi.

Usiache akili zako zifanye kazi zenyewe maana wakati zinaumbwa hazikuumbwa zifanye kazi zenyewe

Ziliumbwa zifanye kazi na ROHO MTAKATIFU pamoja na NENO la MUNGU!

Akili zilizotawaliwa na ROHO MTAKATIFU na NENO uona fursa, uona lililokusudi la MUNGU ktk kila jambo! Uweza kuchambua mawazo ndani na kutekeleza yaliyo ya kusudi la MUNGU ndani yako, utenga lililo baya na kukuweka mbali na akili mbaya!

Ombea akili zako leo, zikabidhi madhabahuni kwa YESU ili zikarabatiwe na kuwa mpya na kuundwa upya

UFALME KWANZA

Naibariki wiki yako
Naibariki Jumatano yako

..."Jesus Up"...

Maoni