Sio kwenye milima wala sio Yerusalem. Mwabudu Halisi anajua kuwa kumwabudu Mungu hakuna mipaka wala umbali na wala sio lazima uwe ndani ya jengo au kanisa au msikiti au hekalu. Baada ya mwanamke Msamaria kutambua kuwa Yesu alikuwa nabii akamuuliza MAHALI SAHIHI PA KUABUDIA. Na Bwana Yesu akamwambia zamani mlikuwa mnaabudia kwenye milima, na wengine Yerusalem ila kuanzia sasa, yaani baada ya mtu kukutana na Yesu na kutambua kuwa Yesu ndio Bwana na mpakwa mafuta basi unatakiwa kujua kuwa hata MFUMO WAKO WA IBADA unatakiwa kubadilika na kufanana na Yesu. Mwabudu Halisi anajua hata chooni ni mahali sahihi pa kufanya ibada na sio lazima awe kwenye jengo la kanisa. Unaweza kufanya ibada popote, unaweza kumsifu Mungu popote, unaweza kumshukuru Mungu hata kama uko kwenye daladala, unaweza kuliitia jina la Bwana ukiwa unatembea barabarani au hata ukiwa kitandani unapolala. Ukijua hili basi mfumo wako wa maisha ya ibada hautasubiri kuhamasishwa na vyombo vya muziki kanisani bali ukifika kanisani vyombo vinakukuta tayari uko mahali sahihi. Ibada kwa Mungu aliye mahali pote inafanywa na Mwabudu Halisi katika roho na kweli. Usijiwekee mipaka ya kumuabudu Mungu kwa kusubiria kwenda tu ndani ya jengo la kanisa,hata hivo kumbuka kuwa wewe ni hekalu na Mungu na Roho wake anaishi ndani yako. WORSHIP TRANSCENDS PHYSICAL BUILDINGS. Heart2Heart Worship Moments by Raphael JL:
Maoni
Chapisha Maoni