HABARI NJEMA KWAKO MTANZANIA

HABARI NJEMA KWAKO MTANZANIA

Fichuka Ndugu Yangu

Je! Unapenda Kusikia Habari Njema, Na kuwa Huru? 

-Ninayo mengi ya Kusema na kuandika, ila kwa haya machache Leo yatakupa Uhuru.

Wakati wa Vita vya Kagera, Mwl. Nyerere aliwaambia Watanzania na Jeshi kwa ujumla juu ya Idi Amini Dada, ya kwamba "UWEZO WA KUMPIGA TUNAO, SABABU YA KUMPIGA TUNAYO NA NIA YA KUMPIGA TUNAYO."

Jiulize Unauwezo gani, sababu ipi na Nia ipi ya kuleta Mabadiliko katika Ulimwengu huu wa sasa ambao thamani ya Utu imepotea. Tajiri amwonapo Maskini anaona Pesa badala ya kuona kiumbe wa Mungu.
-Anajua Akimfanya Kahaba atapata Pesa, Anajua akimfanya Begi la Kubebea Madawa ya Kulevya atapata Pesa.
-Wewe uliye Kijana, ndiye mwenye kuleta Mabadiliko Chanya katika Ulimwengu huu kuanzia Chuoni au hapo ulipo.

Mungu kawekeza vitu vya thamani ndani ya kila Mtu, huyo uliyeketi naye hapo anavitu vya thamani na vya kipekee sana ndani yake. Kwasababu unapenda sana kuwahukumu watu kwa Kuangalia maisha yao ya Leo, ndiyo maana haufaidi Madini yaliyo ndani yao.

Leo FICHUKA. DISCOVER YOURSELF IN GOD. Unavyomjua Mungu zaidi, ndivyo Unavyojijua wewe na kuwajua wengine. Huwezi Kujitambua vizuri nje ya Mungu.

Kama Mimi NilivyoFICHUKA, Napenda nawe Ufichuke ndani ya Mungu.
-Ukifichuka Utakuwa Huru. Watu watakuhukumu kwa Kuangalia umbo lako, kabila lako au mahali unakotoka kama walivyofanya kwa Bwana Yesu wakidhani ya kwamba Neno jema haliwezi kutoka Nazareti.
- Kumbuka hakuna aliyeandika Barua ya Kuzaliwa jinsi alivyo au Kuzaliwa na Wazazi fulani.

Njia kubwa ya KUFICHUKA ndani ya Mungu ni kwa KUVISOMA VITABU.

 Kusoma Vitabu siyo Kipaji, ni Tabia inayotengenezwa na Mtu mwenyewe kila Siku (Lackson Tungaraza).

-Kwa kuvisoma Vitabu, Danieli alifahamu hesabu ya Miaka ambayo neno la Bwana lilimjia Nabii Yeremia, ya kuutimiza Ukiwa wa Yerusalemu, yaani miaka Sabini (Dan 9:2).
-Wachawi na waganga pia husoma Vitabu, na ndiyo maana wanaufahamu mkubwa wa Kuteka Fikra za Watu(Matendo Ya Mitume 19:19). Je!Wewe unasoma nini?

💉Hakuna aliyewahi kuleta mapinduzi chanya Ulimwenguni bila Kusoma Vitabu.

🔦Nina Kitabu hapa Kitakachokutoa Mafichoni na Kukuweka Hadharani/Nuruni. Kinaitwa FICHUKA (Discover Yourself in God). 
-Kina Sura 10, ambazo ni;

1: Shauku Ya Kujitambua

2: Nguvu Ya Kuzaliwa -(Tambua kwanini Ulizaliwa jinsi ulivyo, na zaidi)

3: Nguvu Ya Uwepo Wako-(Kwanini bado tunakuhitaji duniani)

4: Vumbua Kazi ya Mungu ndani Yako -(Jambo ambalo Mungu kakuumba ili ulifanikishe, nalo likufanikishe)

5: Vumbua nani wa Kuambatana naye -(Siyo kila Mtu ni wa kwako)

6: Kabla ya Kuoa au Kuolewa -(Mambo Ya Kujifunza na Kuzingatia zaidi)

7: Fichuka kama Mbegu-(Hatua za Kufuata ili Ukue na Kufanikiwa baada ya KuFichuka)

8: Udanganyifu wa Moyo -(Kujua namna ya Kushughulika na Moyo wako Uliomdanganyifu kuliko Vitu vyote, na wenye ugonjwa wa Kufisha)

9: Chagua Kujiamini -(Building Confidence in yourself)

10: Acha Alama -(Mambo ya Kufanya na Namna ya Kufanya ili uache Kumbukumbu yako kila mahala unapokwenda duniani)
#HAMU YÀKO YA KUTAMANI KUJITAMBUA, NDIYO MSINGI WA KUJITAMBUA.!

🎀-KITÀBU Kina Kurasa 308 tu, ambazo ni chache kuliko tamthilia za Kihindi unazoangalia, na hivyo naamini Utakisoma Chote na Kujifunza Mengi. Kurasa za Kubadili Maisha Yako daima.

🎗 KINAUZWA KWA GHÀRÀMÀ NDOGO SANA YA TSH.20,000 tu. Gharama ndogo kuliko Ya Kugharamia Starehe ya Muda mfupi Gesti au Klabu.

BONUS: Utaungwa kwenye Kundi la Whatsapp ambapo Tunajadili Sura zote za kwenye Kitabu, Kukuelewesha Ulipokwama.

🍒Tumia Namba ifuatayo Kupata Kitabu popote pale Ulipo; 📞0767 033 300

Ubarikiwe Sana, Uwe na Maishà ya Viwango.

Maoni