Salamu kwako msomaji.
Jesusu Up!
Moja kati ya utajiri aliopewa Lucifer
ambae kwa sasa ni maarufu sana kwa jina la Shetani au Ibilisi au baba wa uongo,
ni muziki. Tukimuongelea Lucifer tunamuongelea
jamaa fulan hivi anaemjua Mungu kuliko sisi. Jamaa fulani hivi ambae anamjua
Mungu sio kwa kupitia neno au maombi au kufunga na kuomba. Anamfahamu Mungu kwa
kukaa nae na kumtumikia kwa muda wote mpaka pale biashara ya UCHUUZI
ilipomletea hasara kubwa sana mpaka kuondolewa kwa nguvu edeni. Kwa maelezo ya
kina kuhusu huyu jamaa unaweza pata muda Ezekiel
28 na Isaya 14. Soma kwa makini
na uone kuwa adui yetu sio adui wa kawaida, ni mbunifu wa uharibifu na
mwanzilishi wa kuiga kazi nzuri zote za Mungu na kuzifanya za kwake. Kikubwa
kuhusu huyu jamaa ni kwamba ana HILA na za kutosha kwani siku zote ametaka na
kutamani kuchukua nafasi ya Mungu kwenye maisha ya wanadamu baada ya kushindwa
kuipata nafasi hiyo kwa malaika wenzake. Lucifer alikuwa malaika mzuri na
mwenye uzuri kuliko malaika wote, alikuwa na hekima na uzuri na kimsingi yeye
ndo alikuwa KIPEO CHA UZURI NA UKAMILIFU. Naomba kwa sasa nichukue kipande
kimoja tu ili nizungumze ninalotaka kusema. Lucifer aliumbwa na vinanda, vinubi
au kwa lugha ya sasa aliumbwa na vyombo vya mziki na ndio maana watu wengi
husema alikuwa akiongoza ibada ya uimbaji huko. Okay, niendelee sasa.
Kama wewe ni mwanamuziki
au mwimbaji basi jikaze tujifunze
wote mpaka mwisho na hata mimi ninasema nikijuacho kwa sehemu ya uelewa wangu
na kwa hiyo ukiona kuna kitu kinapungua ujue kwangu hakipo kwani tumepewa kwa
sehemu tu. Mpaka sasa muziki unaonekana kusimama katika nafasi kubwa sana ya
kuwaunganisha au kuwatengenanisha watu ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha kwa
ujumla wake. Kabla sisi huku duniani hatujaanza kuimba au kupiga vyombo ni
muhimu kujua kuwa muziki na uimbaji wenyewe ulikuwepo tokea enzi za malaika
kuumbwa na ushahidi ni kama huo nimeonyesha. Kimsingi, ni Mungu ndiye alieweka
IDEA au WAZO la kuwa na muziki au uimbaji kwa mara ya kwanza kwani wote, yaani
Lucifer pamoja na vyombo vya muziki alivyoumbwa navyo havikujiumba vyenyewe.
Hili ni kubwa sana kulijua. Ingawa lipo la pili la kujua hapo hapo. La pili ni
kwamba, muziki kama tunavyoujua sasa sio mziki wote tulionao sasa umetoka kwa
Mungu ingawa pia sijui ni style ipi au aina ipi ya muziki ila najua jambo moja
kuwa baada ya Lucifer KUTOKA KWENYE UWEPO WA MUNGU kila kitu alichokuwa nacho
KILIHARIBIKA.
Kuelewa hilo la juu ni muhimu ukaelewa hili nisemalo hapa sasa.
Ni hivi, baada ya Lucifer kufukuzwa toka Edeni, hakunyang’anywa vile vipaji
aivyopewa, yaani hakunyang’anywa muziki na vyombo vyake. Ila kuna kitu kimoja
kikubwa aliondolewa. Kitendo cha kuondolewa EDENI, maana yake aliondolewa
kwenye UWEPO WA MUNGU.
Kitendo hicho ambacho kilisababishwa na MAJIVUNO NA KIBURI
kwa kuwa alikuwa mzuri na alikuwa na hekima na alikuwa na vipaji lukuki.
Alipoondoka tu kwenye UWEPO WA MUNGU basi kila alichoondoka nacho KILIHARIBIKA,
yaani hakikufaa tena kwa matumizi ya kumtukuza Mungu kwani HUWEZI KUMTUMIKIA
MUNGU KWA KIPAJI KILICHO DHAMBINI au huwezi kutumia kipaji chako kumtumikia
Mungu na huku kitendo cha kwamba umetoka UWEPONI MWA MUNGU kinaharibu hata
kipaji chako kufaa mbele za Mungu. Nitaelezea kwa kina hapa tuelewe.
Itaendelea…
By Raphael JL:
0767033300.
Maoni
Chapisha Maoni