YKM DAR ES SALAAM - KINGDOM CHARITY AT MSIMBAZI MATERNITY CENTER



YKM DAR ES SALAAM - KINGDOM CHARITY AT MSIMBAZI MATERNITY CENTER

Kama ilivyo moja kati ya huduma tisa (9) zilizopo ndani ya YKM ambayo ni KINGDOM CHARITY yenye kauli mbiu isemayo Impacting through giving/ Kubadilisha maisha ya jamii kupitia utoaji. Hii inapatikana katika kitabu cha Matendo ya Mitume 20:35.
“35 Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea.”

KINGDOM CHARITY inahusika na kuwafikia na kuwagusa wahitaji mbalimbali katika jamii na kuwaonyesha upendo wa Mungu kupitia utoaji.

Mnamo tarehe 12/01/2017 siku ya Alhamisi YKM DAR ES SALAAM ilifanya tendo la Upendo kabisa yaani CHARITY katika kituo cha kulelea watoto wasio na wazazi (au mzazi mmoja) cha MSIMBAZI MATERNITY CENTER. Kituo hiki hulea watoto kuanzia siku moja mpaka miaka mitatu, na baada ya hapo huamishwa kituo kwa ajili ya malezi zaidi. YKM DAR ES SALAAM ilipata kibali cha kutoa msaada/sadaka ya vitu kama sukari, sabuni, biskuti, mafuta na kwa kiwango kikubwa Pampers pamoja na maziwa ya lactogen kwa kuwa wengi wao ni watoto wadogo sana. Vitu hivi walivikabidhi kwa wahusika na kupokelewa kwa furaha.

 
  



YKM DAR ES SALAAM  walipokelewa vizuri na kutambulishwa pia kuonyeshwa mazingira ya kituo hicho ambapo walipata fursa ya kupiga picha na kucheza na baadhi ya watoto wale wenye umri wa kati yaani chini ya miaka mitatu.

 

      


YKM DAR ES SALAAM pamoja na watoto wote pia walipata nafasi ya kusherehekea kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa yaani BIRTHDAY ya dada Nyarobi Nkwimba ambaye alitimiza miaka kadhaa siku hiyo. Dada Nyarobi aliona ni vyema kwenda kusherehekea pamoja na watoto hawa kama moja kati ya jambo la kuwafurahisha na kuonyesha upendo kwa watoto hawa.

                                 


Mwisho ni Shukrani za dhati kwa Kiongozi wa charity mkoa wa Dar es salaam Ndugu TOP KASORO kwa maandalizi mazuri aliyoyafanya na kufanikisha tukio hili ambalo kwetu ni agizo la YESU mwenyewe. Pia shukrani kwa wale wote ambao walijitoa katika kuwawakilisha YKM DAR ES SALAAM, ambao ni
1. VIOLETH BURA
2. JULIETH WINSTON
3. STEPHEN MUNISS
4. ELIBARIKI KIVUYO
5. PRAYGOD SARAKIKYA
6. REBECCA YONA
7. NYAROBI NKWIMBA
8. EMANUEL AMON
9. KELVIN DANFORD
10. REINA HEPELWA
11. ANNA TUPA
12. RONALD FOYA
13. GRACE MASANJA
14. UPENDO SENI
15. GWAMAKA MWASOMOLA

  

Tujitoe katika kumtumikia Bwana

MUNGU AWABARIKI
MUNGU IBARIKI YKM


2017_USHIRIKA_NA_MUNGU

Maoni