SIKIA UPONE


Quotes by Raphael JL: Raphael, uwe makini sana. Unaweza ukawa umeandika mashairi yenye Mungu kabisa, lakini muziki utakaopigwa au melody yake inaweza ika imetengenezwa au kuchukuliwa kutoka kwenye nyimbo za Michael Jackson...kitakachotokea utabaki na mashairi yako mazuri lakini watu watasikiliza zaidi muziki kwani huo mchanganiko haukubaliki. Kwani husikii kuna nyimbo zinaitwa ZA INJILI lakini ukisikia muziki wake unaona kabisa vipande vya kanda bongoman?

Uwe makini na KACHUMBARI YA NYIMBO ZA INJILI. Ukiona huwezi kutofautisha kati ya ROMANTIC LOVE SONG AND WORSHIP SLOW SONG ujue umevaa koti la upupu.

Naona siku hizi unatunga nyimbo kwa kuangalia SOKO ndo maana nakuonya usije ukavalishwa sketi siku unapokea tuzo ya muimbaji bora wa nyimbo za injili huku umepakwa wanja na lipshine na wewe nij mkaka. Raphael, usinichukie kwa kukwambia ukweli,nataka upone. EFATHA RAPHAEL.
Ushirika na Mungu!

Maoni