Na huu ndio uzima wa milele: wakufahamu wewe ambaye pekee ni Mungu wa kweli, nakumfahamu Yesu Kristo ambaye umemtuma.
And this is eternal life, that they may know You, the only true God, and Jesus Christ whom You have sent.
Maneno haya yana nguvu ya ajabu. Ya KWELI ndani yake. Bwana Yesu anaelezea nini maana ya uzima wa milele ambao tunaupata kwa kumuamini yeye na kumpokea na kumkubari kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yetu. Hii ndio maana ya UZIMA WA MILELE, ni lazima kumjua Mungu.
Ni lazima kujua kuwa huyu Mungu ni wa pekee na ni Mungu wa kweli. Ni Mungu wa pekee, yaani hakuna mfano wake wala hakuna anaefanana na yeye. Ni Mungu asiesema uongo, ni Mungu wa kweli. ni lazima ujue kuwa Mungu YEHOVA ni Mungu wa pekee na wa kweli. pia ni lazima umjue Yesu Kristo aliyetumwa na Mungu kuja kutukomboa na dhambi zetu. Njia rahisi zaidi ya kumjua Mungu ni kumjua Yesu Kristo aliyetumwa kwani Bwana Yesu alitumwa kumdhihirisha Mungu asiyeonekana kwa macho ya kawaida. Huu ndio Mkate wa Uzima leo, fichuka ulikofichwa na uufungue moyo wako na kumpokea Bwana Yesu ndani ya moyo wako naye atafanya makao kwako. Ni raha ya namna gani hii.
CHORA MSITARI LEO,kaa mbali na dhambi. Bwana Yesu ndiye Mkate wa Uzima, yaani NENO lake.

Maoni
Chapisha Maoni