HEART 2 HEART WORSHIP- THE FOCUS IS GOD
Moja kati ya mambo ya msingi kabisa ambayo unatakiwa uyajue na kuyafanyia kazi kama Mwabudu Halisi ni kutokupoteza FOCUS.Yaani unaabudu nini au unamwabudu nani au machi yako na moyo wako na nia yako inaabudu nini. Any time God Jehova is not the FOCUS of your worship you are just worshiping idols. Inaweza ikawa pesa zako ama nyumba yako ama miguu yako ama mke au mume wako au watoto wako au umbile lako au sura yako au simu yako au whatsapp na instagram yako. Utajuaje FOCUS sio Mungu aliye hai? Angalia muda unaotumia. Angalia CONCENTRATION yaani mkazo unaoweka ukitumia hivo vitu ukilinganisha na ukiwa unafanya vya Mungu. Unatumia muda gani kuomba ukilinganisha na muda unaotumia kuangalia DP za watu? Unatumia mkazo na muda gani kusoma NENO ukilinganisha na muda unaotumia kusubiria msg mpya inbox? Unatumia muda gani KUTAFAKARI NENO ukilinganisha na muda unaotumia kutafakari nini cha kuandika as a new status FB? IF GOD IS NOT THE FOCUS,UNAABUDU SANAMU. Mwabudu Halisi anajua kuwa NOTHING ELSE QUALIFIES AND DESERVE OUR WORSHIP THAN GOD ALMIGHTY. Jipime. Jikague. Jichunguze. Mwabudu Halisi ANAJUA ANAEMWABUDU. Heart2Heart Worship Moments by Raphael JL:
Hakuna maoni: