HEART 2 HEART WORSHIP- TRUE WORSHIP START FROM WITHIN


Mwabudu Halisi ni HEKALU LA MUNGU na ROHO wa Mungu anaishi ndani yake. Kumbe hapo hekaluni ndio mahali sahihi pa ibada kwani Roho wa Mungu anaewezesha maisha ya mwabudu yawe hai yuko ndani yake. Ndani ya hekalu ndiko mahali sahihi pa kuishi maisha yote ya kumuabudu Mungu kwani ili mradi bado uko mwilini basi MWILI WAKO NI HEKALU NA MUNGU. Mwabudu Halisi hasubiri kwenda kwenye jengo la kanisa au msikiti ili aabudu au ili afanye ibada bali anajua yeye mwenyewe ni A MOBILE WORSHIP TEMPLE na kwahiyo hata akiwa kwenye daladala au chooni au kwenye basi au ndege au bajaji anaweza akaendelea na ibada yake. Kumbuka tunapokutana pamoja kwenye kusanyiko huwa zipo taratibu zilizowekwa ili kutusaidia kufanya mambo kwa umakini ila mimi na wewe tunatakiwa tuwe tunaishi maisha ya ibada hata kabla au baada ya kutoka kanisani au msikitini. Moja kati ya kazi kubwa alokuja kuifanya Bwana Yesu ni kuhamisha MAHALI pa kufanyia ibada kutoka kwenye milima au Yerusalem mpaka NDANI YA MOYO WAKO. (Yohana 4:22-24) Hii ina maanisha ibada ya kweli inaanzia na kuishia ndani ikimlenga Mungu. TRUE WORSHIP STARTS FROM WITHIN, kumbuka ni huko ndiko ziko CHEMCHEM ZA UZIMA. Kwahiyo ukitaka kuwa mwabudu halisi ni lazima utakuwa makini sana kuweka mazingira yako ya ndani vizuri. Usisahau kuwa WORSHIP IS ABOUT GOD. Heart2Heart Worship Moments by Raphael JL:

Maoni

  1. Enter your comment...Me Alex, I come to realize that .....in order to create that spirit of H2H WORSHIP MOMENT in life of a Christian I must be close to Jesus (Abide in him). Giving a high priority to my deeds to Jesus himself because he is the vine and am the branches, i must depend on him in oder to bear good fruits that's WORSHIP EXPERIENCE IN OUR LIFE.
    James 4:4 ..."friendship with the world is an offence to God"....... hahaaaaa the solution is heart to heart worship moment business.

    JibuFuta

Chapisha Maoni