HEART 2 HEART WORSHIP- USIJICHANGANYE



⁠⁠⁠
USIJICHANGANYE-USICHANGANYWE ukakosea kuelewa kuwa yapo mambo ambayo ukifanya yanadhihirisha kuwa unamwabudu Mungu wa kweli Yehova ama unaabudu vitu vingine. Fahamu kuwa hata wanaoabudu sanamu pia hutoa sadaka, huimba na kuongea maneno mbele ya madhabahu za miungu yao. Kwa mfano kutoa sadaka ni sehemu ya ibada, kuimba ni sehemu ya ibada, kusaidia masikini ni sehemu ya ibada na changamoto ni kwamba hata wanaomwabudu BAALI wanafanya hayo mambo. Utofauti upo kwenye anaeabudiwa na anaeabudu. Mungu wa kweli yaani Yehova ndiye Mungu wa pekee na wa kweli (Yohana 17:3) na pia ndiye muumbaji wa vyote. Utofauti utaonekana katika namna ambavyo Mungu wako ATAJIDHIHIRSHA NA KUKUJIBU NA KUTIMIZA MAPENZI YAKE katika ibada ya maisha yako kinyume na wale waabuduo mizimu na wafu. Kama kweli Mungu unaemwabudu ni wa kweli HATAKAA KIMYA. Unakumbuka Mungu wa Elia alivyojibu kwa moto? Kizuri Mungu wa Elia bado ni Mungu wako na wangu.Mwabudu Halisi anajua Mungu wake lazima atatokezea tu hata kama ni kwenye kutoa sadaka au kucheza kama Daud. THE FOCUS OF WORSHIP IS JEHOVA. Heart2Heart Worship Moments by Raphael JL:

Maoni