MKATE WA UZIMA


MKATE WA UZIMA- MSIIFUATISHE NAMNA YA DUNIA HII: Warumi 12:2 inasema msiifuatishe NAMNA YA DUNIA HII, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya NIA zenu. Ndipo mtakapoweza kujua na kuonja na kuhakikisha NI NINI MAPENZI YA MUNGU yaliyo MEMA, YANAYOPENDEZA machoni pake na UKAMILIFU. Wazo ni hili, ulimwengu huu una mfumo wake wa maisha, mfumo wa nyimbo na uimbaji na muziki, mfumo wa mavazi, mfumo wa matamshi au kuongea, mfumo wa kuoa na kuolewa, mfumo wa kuenenda. Na pia kwamba LIFESTYLE ya ulimwengu huu iko tofauti sana na ile ya UFALME WA MUNGU. Hapa tunahamasishwa kuwa waangalifu na kuacha kuifuatisha NAMNA YA DUNIA. Basi jitazame ulivyovaa, angalia hizo nguo zako, angalia unavyoongea, hebu JIKAGUE uone unavyowaza na unavyoenenda mbele ya wengine. Check ushuhuda wa maisha yako. KUMBUKA:Ni vigumu sana kujua MAPENZI MEMA ya Mungu kama bado utakuwa unaifuatisha NAMNA YA DUNIA HII. Leo unaweza kufanya maamuzi. WEWE NI CHUMVI NA SIO SUKARI.

Maoni