- MUNGU KWANZA, hii ni kauli mbiu na wito kwa wana YKM wote ulimwenguni, popote walipo na chochote wanachofanya.
- Tunajifunza Mathayo 6:33 kuutanguliza KWANZA UFALME WA MUNGU NA HAKI YAKE kwani mengine tumeambiwa tutazidishiwa.
- Haimaanishi mengine hatuyatafuti bali hatuyapi kipaumbele cha kutufanya tukose raha, tukose amani kwa sababu yake. Bali tunatanguliza kwanza Ufalme wa Mungu na Haki yake, yaani MUNGU KWANZA
- Amosi 3:3 inasema je, watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana? Katika maisha yako ya ujana ni muhimu sana kukusudia kuambatana na kutembea na Mungu kwa makubaliano na mapatano.
- Kutembea na Mungu maana yake kuishi katika ushirika na Mungu, maana yake ni kuishi ukijua kuwa hauko peke yako.
- Kama kweli ukikusudia kutembea na Mungu kila siku basi ni lazima ukubali kubadili mfumo wako wa maisha kwani huwezi kutembea na Mungu kama unatembea na mjomba wako.
- Huwezi kutembea na Mungu ukamfaidi kama hata Mungu mwenyewe humjui, ni muhimu sana kumjua Mungu maana hapo ndo sehemu ya kuanzia.
Usikose kuwepo
Usikose nakala yako
38 DAYS LEFT
30/10/2016
Mratibu wa Fichuka.
Musa Joseph
0717720072

Maoni
Chapisha Maoni