Ads Top

PAKUA UWEZO/FICHUKA- HATMA YANGU NI UWEPO WA MUNGU


HATMA YANGU NI UWEPO WA MUNGU

Maisha ya Ibada yanahitaji mambo haya;
1.  Ni lazima ujue na ukubali kuwa unaemuishia maisha hayo ni Mungu, yaani maisha ya ibada kwa Mungu ili kwamba yeye akutumie vile apendavyo kama dhabihu takatifu ilotolewa kwake.
2. Ni lazima ukubali kulipa gharama ya kumsikiliza sana Mungu kupitia Neno lake, hapo lazima ukubali kuwa mpenzi wa karibu wa biblia ili uisome, uisikilize, uielewe na uzidi kuyaweka maneno hayo ndani yako.
3. Wewe ni hekalu la Mungu na Roho wake Mtakatifu anakaa na anaishi ndai yako na kwahiyo huna sababu ya kujitetea kwanini haiwezekani. Lile neno ulilojaza ndani yako ndio kitanda cha Roho Mtakatifu, ndio makazi sahihi ya Roho Mtakatifu na ndio njia ambayo utaitumia kujenga na kuimairisha ushirika na Mungu kupitia Roho Mtakatifu.
4. Mwabudu halisi tayari ufahamu wake unakuwa umebadilishwa kwa kufanywa upya na nguvu za Roho Mtakatifu aliye ndani yake. Nia yake iko sawa na sahihi, hana hila wala unafiki wala majungu. Yeye anachukia dhambi na ndo maana hawezi kujichanganya.

Usikose kuwepo
Usikose nakala yako
32 DAYS LEFT
30/10/2016

Mratibu wa Fichuka.
Musa Joseph
0717720072
http://fichuka.blogspot.com

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.