Ads Top

TAFAKARI YA SIKU- JUMATANO


 Ambassador of Christ
YESU Asifiwe..

Daka hii..

"N'nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri ktk upole wa hekima" Yak 3:13

Nje ya NENO la MUNGU hakuna ufahamu wala hekima, nje ya ROHO MTAKATIFU vivyo hivyo hakuna ufahamu wala hekima! Vyote hivi utekelezwa na FIKRA ndani ya mtu kwa hyo FIKRA zako zikitawaliwa na NENO la MUNGU na ROHO MTAKATIFU automatically ufahamu wako utaongezeka, hekima kwako itaongezeka tena yenye kujaa Neema ya KRISTO. Huwezi kutenda hekima au maarifa kwa kutumia akili zako mwenyewe maana akili ziliumbwa zifanye kazi na NENO la MUNGU na ROHO MTAKATIFU! Na ile hekima ya MUNGU ndani yako ujaa sifa.hizi:-
â–¶ Kwanza ni safi
â–¶ Tena ya Amani
â–¶ Ya Upole
â–¶ Tayari kusikiliza maneno ya watu
â–¶ Imejaa Rehema na matunda mema
â–¶ Haina fitina
â–¶ Haina unafiki

Tamani kujaa hekima na ufahamu utokao juu. Tamani kuona kila iitwapo leo unasogea ktk viwango vipya ktk FIKRA zako! Tamani kumsihi MUNGU ktk TOBA pale ambapo ukufanya sawasawa ktk kutimiza kusudi alilokupa! Tamani kuona unafanya kazi pamoja na ROHO MTAKATIFU na NENO LA MUNGU ili utembee ktk hekima na ufahamu utokao juu wala si wa dunia hii ambao ni batili

UFALME KWANZA

Naibariki wiki yako
Naibariki Jumatano yako

..."Jesus Up"...

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.