Ads Top

HEART 2 HEART WORSHIP- MWABUDU HALISI NI HEKALU LA MUNGU


Wewe Mwabudu Halisi ni HEKALU LA MUNGU, kwahiyo huwezi kuvaa nguo kama zile sanamu za kujaribia nguo zinazowekwa nje ya maduka ya nguo. Mwabudu halisi anajua kuwa yeye kama HEKALU LA MUNGU anatakiwa kujua kuwa kwanza kabisa huo mwili au hilo hekalu sio mali yake na kwahiyo hatakiwi kuvaa nyavu za kuvulia samaki na kuuacha mwili wake kama jalala linalotupiwa kila aina ya uchafu. Kama uvaaji au nguo zisingekuwa na umuhimu wowote ni wazi Mungu asingetoa maelekezo ya nguo za mwanaume na nguo za mwanamke ndani ya neno lake. Pia kungekuwa hakuna haja ya Mungu kujaza maelezo ya nguo maalum za makuhani wawapo katika ibada,angeruhusu basi hata wavae bukta na OPP. Sasa ni hivi, wewe usihangaika, kama sio kuhani unaweza kuvaa vyovyote vile maana humuhudumii Mungu bali FASHION.Hapo ni angalizo kwani kwa jina la FASHION watu wamekuwa kama vichaa, ni kweli unataka kuvaa nguo inayobana ili uonyeshe figa yako lakini kuhani anajua figa yake sio ya maonyesho. Kumbuka pia kuwa hata mapaja yako ambayo huwekwa wazi kwa njia mbali mbali ikiwemo mipasuo ina matumizi yake, ni hatari kwa Mwabudu Halisi kuleta chakula cha PRIVATE, PUBLIC. Ingekuwa hivo basi ni bora kutembea na kumwabudu Mungu ukiwa uchi, yaani kama umeamua kuvaa vibaya ni bora uvae vibaya mazima ili ijulikane kuwa umeamua kuwa hivo. Ukiwa ndo kiongozi wa uimbaji na umevaa vibaya na huku unataka kuinua mikono yako juu ujue wewe ni SUKARI na sio CHUMVI. Je, HAMJUI YA KUWA MIILI YENU NI HEKALU LA MUNGU? Kumbuka ibada ya kweli inafanywa ndani ya hekalu yaani mwili wako na hivyo jifunze kuutoa mwili wako kama sadaka, dhabihu takatifu kwa Mungu maana hiyo ndiyo ibada yako yenye maana. Ni kweli Mungu anaangalia moyo ila hakuwaacha Adamu na Eva watembee uchi baada ya kutenda dhambi. ZINGATIA. THE FOCUS OF WORSHIP SHOULD REMAIN TO BE GOD. Heart2Heart Worship Moments by Raphael JL:

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.