HEART 2 HEART WORSHIP- UTAJUAJE UNAABUDU KITU KINGINE


Utajuaje unaabudu kitu kingine na sio Mungu Yehova? Utajuaje unaabudu sanamu? Utajuaje unaabudu mitandao ya kijamii? Utajuaje? Mwabudu Halisi anajua fika kuwa muda hupangwa kwa kuangalia kipaumbele na umuhimu wa jambo. Kama huwezi kutoa muda wa kumtafakari Mungu wako, huna muda wa kuomba wala kusoma neno lake, huna muda wa kuamka na kuomba usiku, huna muda wa kumlingana Mungu wako na ikitokea una muda basi si zaidi ya dakika kumi na tena akili yako inakuwa inatamani uwahi kumaliza. Na huku unaweza kutumia masaa kupiga story na mpenzi wako, unaweza kutumia masaa kuchat kwa whatsapp au facebook au instagram ujue hakika UNAABUDU SANAMU. Unaabudu hicho kinachokulia muda wako mpaka kila unapotaka kufanya jambo la Mungu unaona huna muda, ila una muda wa kuangalia Isidingo, muda wa kuangalia series huo upo hata masaa matatu ila ikija tu hata kuomba unaanza kukoroma na kujiona umechoka. Mwabudu Halisi anajua MUDA ndio kila kitu na ya kwamba jambo lolote unalotoa muda wako zaidi kulifanya LINAKUWA KUBWA NDANI YAKO lakini pia inaonyesha jambo hilo kwako ni muhimu kuliko mengine. Mwabudu Halisi anajua SAA YAJA, NAYO IMESHAKUJA yaani sasa, ya kwamba roho na kweli ndio kipimo cha ibada kwa namna ambayo ndani ya masaa 24 hawezi kukosa MUDA wa kufanya mambo ya ibada kwa Mungu wake. Unalala kama gogo, unaamka kama mti, unakula kama mnyama, bila hata namna ya kuonyesha kuwa unae Mungu ndani ya maisha yako. Mwabudu Halisi anajua HAKUNA JAMBO DOGO AMBALO HALIMUHUSU MUNGU kwani ndani yake JEHOVA tunaishi, tunaenenda na kuwa na uzima wetu. Maisha ya Mwabudu halisi sio ya mkumbo au ya kishabiki kwani yanahitaji NIDHAMU KUBWA YA MTU BINAFSI. Kumbuka, kuongea sana kwenye jukwaa haimaanishi huwa unayafanya unayoongea ingawa hivo ndivo inavyotakiwa. Kuimba sana haimaanishi nyimbo unazoimba ni maisha yako ila ndivyo inavyotakiwa. Ni hatari KUPENDA VYA MUNGU na kumchukia MUNGU mwenyewe. Leo unaweza ukaamua kujipima na kuwa mkweli. Kaa chini utafakari na uone mungu gani anakuharibia USHIRIKA wako na Mungu aliye Hai na kisha uamue leo kubadilika. Ni heri uonekane ANTI SOCIAL kama kuwa social kunakufanya uwe mfuasi wa BAALI. Bado maamuzi ni yako na jambo hili sio jepesi. Nguvu za Mungu za kiwango cha kijiko haziwezi kupingana na nguvu za giza za kiwango hicho hicho na kushinda. Jikague, ukiona unatamani kuacha lakini unashindwa fahamu wazi kuwa UMEVAMIWA na unahitaji msaada kutoka nje maana huenda wewe una nguvu za kiwango cha kijiko. Pima muda wako,kumbuka wote tuna masaa yale yale 24 dunia nzima na kuna watu wako busy kuliko wewe ila uchaguzi ni wako kwani aliyekupa kazi inayokufanya uwe busy hata ukose muda wa kumtambua anayo mamlaka juu ya kazi hiyo,ila maamuzi ni yako. Usipoamua kubadilika sitashangaa sana kwani UTUMWA una raha yake na hasa ukiwa umechanganywa na upumbavu badala tu ya ujinga.TIME INVESTMENT IS A SIGN OF LOVE AND DEVOTION. Heart2Heart Worship Moments  by Raphael JL:

Maoni