PAKUA UWEZO/ FICHUKA- MIPAKA MPAKA KILINDINI
Nguvu ya mipaka kabla hujaoa au kuolewa.
Nini maana ya mipaka?
Mipaka ni sehemu au mahali panapoonesha mwisho wa umiliki halali wa mtu.
Ni sehemu ambapo ndani yake unakuwa na uhalali wa kuweka utawala wako kwa uhuru bila wasiwasi wowote aukuingiliwa na mtu yeyote.
Mungu baada ya kumuumba mwanadamu alimpa mipaka yake ya utawala.
MWANZO 1:26..(Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, nan chi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.).
Hii ndiyo mipaka aliyopewa mwanadamu kutawala vitu vyote katika nchi, angani na baharini.
Mungu alimuumba binadamu kwa kusudi maalumu na kumpa mipaka katika utawala wa vitu vya dunia hii.
Je wewe ukiwa kama kijana ulieumbwa kwa sura na mfano wake Mungu na kubeba kusudi maalumu katika maisha yako unamipaka katika maisha yako?? Au unaishi pasipokuwa na mipaka maalumu juu ya maisha yako, mwili wako, uhuru wako, ujana wako, mahusiano yako,???
Je unatumbua nguvu ya mipaka kwako wewe kijana ambae bado hujaoa au kuolewa??
Je unatumbua faida ya mipaka kabla ya kuoa au kuolewa, Ni kwanini mipaka kabla ya kuoa au kuolewa??
Utawekaje mipaka katika maisha yako kabla hujaoa ama kuolewa???
Usikose kuwepo
Usikose nakala yako
27 DAYS LEFT
30/10/2016
Mratibu wa Fichuka.
Musa Joseph
0717720072
http://fichuka.blogspot.com
Hakuna maoni: