...Inaendelea
Ukaribu baina ya watu ni matokeo, yaani ukaribu hutengenezwa, yaani ukaribu ni hatua endelevu na ya kwamba ukaribu unajengwa na pia unaweza kubomolewa.
Uwezekano mkubwa ni kuwa mambo yale yale yanayojenga yanaweza pia kubomoa ukaribu na tufahamu kuwa ukaribu ukiharibiwa na kubomolewa basi umbali huzaliwa na umbali ukizaliwa maana yake nguvu ya ushaiwishi juu ya huyo mtu inapungua na mwisho kuondoka kabisa.
Ukaribu huanzia mahali fulani, yaani kila mahusiano kuna mahali yalianzia, location. Mlikutania wapi na huyo mtu uliyekaribu nae ina nguvu sana kama nguvu ya mahusiano yenyewe.
Mlikutania wapi. Mlianzia wapi kujenga ukaribu maana ukaribu una mwanzo na huo mwanzo ni lazima ulitokea mahali fulani.
Yaani ni lazima. Mfano, ulikutana nae disco, okay mkakaa pamoja, siku akikwambia aende disco kidogo utashangaa?
Mahali mlipokutania pana maana kubwa sana kwani huwa panatumika kama madhabahu ya kuwaunganisha watu na pia kuwatengenisha.
Fikiria umekutana nae kwenye basi au kwenye ndege au kwenye meli au barabarani ukitembea, ukiangalia kwa kina ni kama nguvu ya mahusiano inategemea sana na wapi mlianzisha mahusiano yenu. Wengine wana historia ndefu yaani wanakaa mtaa mmoja, wamesoma shule moja, wanasali msikiti au kanisa moja, wakasoma chuo kimoja.
Mazingira yanayotukutanisha yana nguvu sana kwani swala hapo sio mazingira tu bali kuna vitu vya ndani yake.
kumbuka
Sababu ya kukutana ina nguvu kuliko mahali pa kukutana. Ni kwasababu hiyo ndio maana ilikuwa ni lazima mkutane hapo.
Kusudi lina nguvu kuliko eneo au mazingira. Mazingira yapo kulitumikia kusudi.
Itaendelea...
Usikose kuwepo
Usikose nakala yako
22DAYS LEFT
30/10/2016
Mratibu wa Fichuka.
Musa Joseph
0717720072
http://fichuka.blogspot.com

Maoni
Chapisha Maoni