Ads Top

TAFAKARI YA SIKU- JUMATATU YA KWANZA MWEZI WA KUMI


Ambassador of Christ
YESU Asifiwe..

Ikiwa ni wiki ya kwanza ya Mwezi na Jumatatu ya kwanza ya Mwezi ni maombi yangu kwa MUNGU juu yako ndani ya Mwezi huu kupitia Mistari ya kitabu cha Warumi kama ilivyoandikwa na Mtume Paul

"_Warumi 12:9-16"_

MUNGU  akakujaze na kukupa ;-

UPENDO WA KWELI
Pendo lenu na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema.

HESHIMA NA KUWATANGULIZA WENGINE
Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;

BIDII NA JUHUDI KATIKA MAMBO YOTE
Kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia BWANA;

TUNDA LA ROHO MTAKATIFU
Kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu; kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni mkijitahidi.

KINYWA NA MIKONO YENYE KUBARIKI
Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani.

UMOJA ULIOJAA UPAMOJA
Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao.

UNYENYEKEVU, UPOLE, FIKRA ZILIZOJAWA NA KUTAWALIWA NA NENO PAMOJA NA ROHO MTAKATIFU
Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili.

BWANA YESU akazidi kukuonekania rafiki, tamani kuzidi kujijenga ktk NENO lake

UFALME KWANZA

Naibariki wiki yako
Naibariki Jumatatu yako

..."Jesus Up"...

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.