Wao wanakusifu wewe kwa kipaji chako,wewe msifu Mungu kwa kukufanya sifa kwa mataifa. Huu ndio mtazamo sahihi wa Mwabudu Halisi,anajua atasifiwa na watu na hawezi kuzuia watu kumsifia,ila pia anajua kuwa hizo sifa anazopewa kimsingi sio zake. Unaposifiwa kwa karama na kipaji chako,usipokuwa vizuri UTACHUUZWA na kuharibiwa na misifa na utakosana na Mungu. Kiburi na majivuno ndio mtaji mzuri wa uharibifu,kumbuka usijaribu kumuweka Mungu kwenye box la kipaji chako,mpe Mungu stahili yake,mpe haki yake. Jenga mtazamo huu,THEY PRAISE YOU,YOU PRAISE GOD. Siku zote usisahau kuwa watu wanaweza kukujaza sifa kwa uzuri na sauti yako ila wewe mtazamo wako ubaki palepale, THEY SEE YOU,YOU SEE GOD. Usikubali kuwa mhanga wa kuchukua sifa za Mungu,kipimo ni hiki,ukimaliza huduma usiposifiwa unajisikiaje? Leo unaweza kubadili mtazamo wako.WORSHIP IS ALL ABOUT GOD. Heart2Heart Worship Moments by Raphael JL:
Mungu Kwanza-YKM!
Maoni
Chapisha Maoni