Ambassador of Christ...
YESU Asifiwe..
Kumbuka hili siku zote rafiki na kamwe usiruhusu mwili wako kutawala roho yako
"Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu" Math 26:41
Usiruhusu mwili kukuletea hali ya kukata tamaa katika kuomba au kukufanya ushindwe kuomba!
Biblia inatuambia kuwa kuingia na kutoka kwetu kwenye majaribuni na changamoto zinazotukumba kunategemea sana kiwango cha maombi tunacho kiachilia juu ya hali hizo!
Kumbuka kuna wakati mwili unachoka sana na kutamani kufanya yake hata wakati mwingine kushirikiana na nafsi halafu vyote vikakubaliana na kuhalarisha jambo kana kwamba ni sahihi na wakati huo roho iko tayari kusikia na kutumika ktk UFALME wa MUNGU na kuwa tayari kuomba hata kuugua juu ya sababu za mwili kuikwamisha kutokuomba!
YESU alitusihi tusiache kuomba maana majaribu ni mengi hatuwezi kushinda kama tunazembea ktk kuomba! Maombi kwetu ni silaha tosha ya kumdhibiti shetani kuharibu,kubomoa na kuvuruga maisha yetu ndani ya KRISTO na nchi yetu hata Kanisa kwa ujumla!
Tukeshe tukiomba pamoja na kufunga maana yapo mambo mengine hayajibiwi bali kwa njia ya kufunga na kuomba!
Tukumbuke roho iko tayari na ina hamu sana ktk kuomba lakini mwili unawekwa vikwazo na sababu nyingii zisizo kuwa na faida ktk kuleta mahusiano yako na MUNGU. Ukiuendekeza mwili mwisho wake ni mauti!!
Prayeeeeeer!!
UFALME KWANZA
Ijumaa yako imebarikiwa ktk JINA LA YESU
..."Jesus Up"...

Maoni
Chapisha Maoni