GHARAMA YA UKIRI-THE COST OF CONFESSION
🔑Kwanza naomba ujue kuwa KUKIRI sio zoezi la kitoto au mzaha, bali ni jambo kuuubwa sana la kiimani.
🔑UKIRI una nguvu,ila nguvu ya ukiri haiko kwenye ukiri wenyewe bali kwenye NIA-ROHO na KUSUDIO linalobeba ukiri wenyewe au linalosababisha ukiri wenyewe.
Mfano Yoshua 1:8-9 inasemaje?
8 Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.
9 Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako
🔑So ukisoma hapo utagundua kuwa NENO LA MUNGU linatakiwa lisiondoke kinywani mwa kila mmoja wetu kwani hilo ndo msingi wa TAFAKARI. Kutafakari ni mchakato mkubwa sana ambao unajumuisha pia KUKIRI. Kukiri ni sehemu ya tafakari. Kadri unavyokiri ndivyo unachokikiri kinazidi kupata nguvu na maana.
🔑KUKIRI kwenyewe hakuna nguvu kama hakutokani na IMANI.
JE, UNACHOKIRI UNAKIAMINI?
JE, UNACHOKIRI UNAKIJUA?
🔑Nguvu ya UKIRI imefungwa ndani ya UADILIFU wa unachokiri,yaani kwamba ukiri wako utakuwa na nguvu na matokeo inategemea sana UBORA WA TAARIFA ILIYOZAA UKIRI WAKO.Ndo maana nasema inabidi UKIRI UTOKE NDANI YA UNACHOAMINI. Kumbuka kufanya jambo lolote lile nje au pasipo imani ni DHAMBI.
🔑GHARAMA YA UKIRI ni kwamba lazima ujue kuwa UNACHOKIRI KITAKUWAJIBISHA. Yaani ukisema mwaka 2017 nitapata kibali lazima ujue KIBALI kipi unazungumzia, lazima ujue unakipataje hicho kibali. MUHIMU SANA HII ndugu zangu.
🔑Mfano: Ukijua kuwa kibali unachokisema ni kile ambacho hakisubirii the approval of men basi lazima ujue kuwa utawajibika kukaa na Mungu ili AKUPE KIBALI mbele zake na mbele za wanadamu.
JE, UKO TAYARI KUISHI MAISHA YA UKIRI WAKO?
🔑Ukikiri kuwa mwaka 2017 utaishi na kutembea kama shujaa, tusije tukakukuta mtaani unatebea kama mtumwa...
🔑Ukisema unataka MTEMBEO WA KIMUNGU 2017, ujue lazima ujue MUNGU anatembeaje, na njia zake ili kwamba usije ukajikuta unatembea kwenye vumbi na huku Mungu yuko barabara ya lami...
DO YOU KNOW THAT EVERY CONFESSION HAS ITS OWN STANDARDS OR PRINCIPLES OR VALUES? JE UNAJUA KANUNI ZA KUISHI NAZO NDANI YA UKIRI WAKO?
Mithali 3:1-4
1 Mwanangu, usiisahau sheria yangu,Bali moyo wako uzishike amri zangu.
2 Maana zitakuongezea wingi wa siku.Na miaka ya uzima, na amani.
3 Rehema na kweli zisifarakane nawe;Zifunge shingoni mwako;Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.
4 Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri,Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu.
🔑Mfano: Ukikiri kuwa mimi NITASHINDA AU NI MSHINDI ujue kuwa washindi wana kanuni wanazotumia kutembea na kuishi. JE, UNAZIJUA?
🔑INAMAANISHA WOTE MNAOKIRI MNA KIBARUA CHA KUVUMBUA HAYA MAMBO KWENYE BIBLIA NA KATIKA USHIRIKA NA ROHO MTAKATIFU.
🔑Hiyo inawahusu wale ambao UKIRI wao unatoka kwenye IMANI...na kama imani hiyo iko GROUNDED, ROOTED AND ESTABLISHED IN THE KINGDOM OF GOD.
So nilitaka tu niwaambie hayo....
Naamini mmenielewa...
🔑So keep confessing lakini tujue TUNAYOKIRI HAYATATOKEA TU KAMA SUPRISE. HATA HIVO IMANI BILA MATENDO IMEKUFA.
🔑Ukisema 2017 is a my year of MAXIMIZING POTENTIAL---Lazima ujue kuwa kuna michakato mingi utkayopitia mpaka kufika hapo ili kwamba utakapotakiwa kupita kwenye njia fulani usikatae na kukimbia. KUMBUKA EVERY GREATNESS IS A FUNCTION OF SERVICE.
🔑IF 2017 HAS TO BE A GREAT YEAR,THEN SOMEONE HERE HAS TO HAVE A GREAT GOD....is someone here with a great God at heart?
🔑KUTEMBEA AU KUJIVUNIA MUNGU MWENYE NGUVU NA HUKU WEWE HUNA AU HIZIONYESHI NI UMASIKINI.
DO YOU HAVE A GREAT GOD?
If you have a great God, then how do you face 2017?
My God is great
My God is powerful
My God is SELF SUFFICIENT
My GOD IS SELF SUSTAINING
MY GOD IS SELF EXISTENT
MY GOD IS THE KING OF KINGS
MY GOD IS AWESOME
MY GOD IS UNPINGIKABLE
MY GOD IS UNKWEPABLE
MY GOD IS A MULTI-SPECIALIST
MY GOD IS OMNIPOTENT
MY GOD IS UNKIMBILIKABLE
MY GOD IS UNTINGISHIKABLE
HE WILL MENTOR ME IN 2017
HE WILL INCREASE ME IN 2017
MUNGU ATANISTAWISHA MWAKA 2017
MUNGU ATANINENEPESHA KWA ASALI NA MAZIWA MWAKA 2017
Mungu akubariki
By
Pastor Raphael JL
Maoni
Chapisha Maoni