UBORA SIO UKAMILIFU WALA USAHIHI



UBORA SIO UKAMILIFU WALA USAHIHI??????

Ni ajabu sana kuwa kanisa linapambana na dunia katika kufanya mambo kwa ubora. Ni ajabu zaidi pale ambapo kati ya hayo maeneo mawili kanisa, ambalo niseme ni KANISA FEKI na sio lile kanisa lilijengwa juu ya mwamba ya mafunuo ya KiMungu,limekuwa linaharibu TASWIRA ya kanisa la ukweli. Na hapa simaanishi kanisa jengo, kwani hata hivo kanisa sio jengo bali MWILI WA KRISTO NA VIUNGO VYAKE.

Sasa ukiangalia kwa makini utaona kuna mambo mengi sana ambayo wale wanaojiita kanisa wamekuwa WANAIGA yale yanayofanywa na WAYEBUSI na WAPEREZI na kuyaingiza kwenye majengo ambayo kanisa hukusanyikia. Wamecopy miziki yao ya humantarian na kuileta. Wamebeba staili za kucheza. Wamebea mavazi huku wakisema MUNGU ANAANGALIA MOYO,na huku wanajua Mungu yuko Mbinguni na huku duniani tuko sisi tunaoangalia kuanzia nje. Wamebeba namna ya shooting za video za WAHITI na kuzileta hekaluni. Wakikuta kazi imefanywa kwa ubora na WAAMORI basi wanaileta na hekaluni. Wanasikiliza nyimbo za WAMIDIANI halafu wanachukua vipande vya Extra Musica na kuvipiga hekaluni.

HUU NI UCHOVU MKUU. HUKU NI KUISHIWA UBUNIFU.

Kwani nani alitakiwa amuige mwenzie?
NANI NI NURU?
NANI NI CHUMVI?
NANI ANA ROHO MTAKATIFU,ROHO WA UBORA NA VIWANGO?


KUTUMIA VIWANGO VYA DUNIA,KUHUKUMU VIWANGO VYA KANISA NI UHUNI WA CHONGO KATIKATI YA VIPOFU.

Kanisa linatoa kitabu na kukiuza 50,000. Ukikipeleka tu sokoni na ukamwambia mtu bei yake anastuka kwanza,anaona ni gharama sana na huku alinunua kitabu cha NJIA SABA ZA MAFANIKIO CHA KAYOSAKI KWA 90,000 na hakuona shida. Mkakati ni kuendelea kuuza vitu vya 5,000 eti eeee???

Mpaka watu wanaogopa kutoa DVD zao za GOSPEL maana anajua akiuza 10,000 atahojiwa tu.

NI HATARI SANA KWA CHONGO KULAZIMISHA URAIS KATIKATI YA VIPOFU.


Kwaheri 2016 mdogomdogo.
By Raphael JL:

Maoni