UMUHIMU WA SIFA NA SHUKRANI



UMUHIMU WA SIFA NA SHUKRANI

KEY VERSE: Zaburi 100:4, Waebrania 13:15.

Zaburi 100:4
Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru;Nyuani mwake kwa kusifu;Mshukuruni, lihimidini jina lake;

Waebrania 13:15
Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamayo jina lake.

🔑 Watu wengi hawajui umuhimu wa sifa na shukrani. Ama wanajua ila wanapuuzia na kupotezea thamani yake. kama ni kutokujua, yaani UJINGA ni jambo linalofundishika na mtu anabadilika. Kama wanapuuzia na kupotea kile wanachojua basi UPUMBAVU umepata ubini wake. Naomba niseme machache kuhusu haya mambo mawili makuu sana.

🔑 Ninaamni kuwa kupuuzia jambo hili la sifa na shukrani kunaweza kukahusishwa na mapokeo pia. Na hasa mapokeo yanayoonyesha kuwa KUSIFU ni kuimba au ni muziki na sio tu muziki ila kusifu ni aina ya nyimbo za haraka haraka. HUU NI UPOTOSHAJI WA AJABU SANA.

🔑 Hili pia linaenda sambamba na kuabudu jinsi inavyochukuliwa kuwa ni nyimbo za polepole na kuwafanya watu kuwa kama waganga wa kienyeji. Kumbuka hata waganga wa kienyeji kabla hawajafanya matambiko yao HUIMBA NYIMBO. So issue hapa sio tu nyimbo au kuimba au muziki. Ni vizuri kupanua ufahamu na kujua namna ya kuelewa mambo vizuri.

🔑 Ukisoma biblia utaona kuwa SIFA NA SHUKRANI sio LITURUJIA YA UIMBAJI bali KIINI CHA FUNGUO zinazomfanya mtu apate kibali mbele za Mungu wake. Kusema sifa ni kuimba ni kiwango cha juu sana cha dharau kwa neno hili. Na ndio maana nadhani kumekuwa na SHOO nyingi za KUBURUDISHA badala ya KUBADILISHA kwani SIFA NI KITI CHA KUKALIA CHA YEHOVA MUNGU WETU.

Zaburi 100:4...inasemaje?

Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru;nyuani mwake kwa kusifu;mshukuruni,lihimidini jina lake

Okay...ukisoma Zaburi 100:4 unaweza usielewe kama huna ufahamu kuhusu HEKALU.
Niseme kwanza moja kubwa hapa...

🔑SIFA NA SHUKRANI NI AINA YA DHABIHU. NOTE THAT.

🔑 Usipokuwa unatoa sifa na shukrani kama DHABIHU utaishia tu kuongea maneno mengi kwakuwa hujaimba.
Kutokuimba haimaanishi hujasifu au hujashukuru, kwani MDOMO HAUNA KAZI YA KUIMBA PEKE YAKE.

🔑 Hekalu lilikuwa na MALANGO-GATES na NYUA-COURTS mahali  ambapo SACRIFICE -DHABIHU-SADAKA zilikuwa zinatolewa. Picha yake ni hii ya kusema unapoingia au unapoenda mbele za Bwana Mungu wako, njia ya kuingia ni SHUKRANI kama dhabihu ya shukrani. Kumbuka kwakuwa sisi ni wapokeaji wa REHEMA NA WEMA WA MUNGU basi kila saa lazima tupeleke dhabihu ya shukrani.

🔑 Pia kuingia nyuani mwake kwa SIFA, yaani kuelezea uzuri wa Mungu. Kumsifu na kumtukuza kwa kuliungama jina lake kuu. Ukichanganya SIFA NA SHUKRANI zitakupeleka alipo MZEE WA SIKU yaani PATAKATIFU PA PATAKATIFU..

🔑 So shukrani na sifa ni FUNGUO za kukuingiza.

Barikiwa 

Jesus Up

Maoni