THAMANI YA KUMTUMIKIA MUNGU UKIWA BINTI
THAMANI YA KUMTUMIKIA MUNGU UKIWA BINTI
Tafsiri:THAMANI ni uzuri au ubora au wema au utukufu ambao kwa context ya somo letu utaupata kwa KUMTUMIKIA Mungu. Kumtumikia Mungu ni kuishi maisha ya KUMJUA,KUMWAMINI na KUINGIZA KWENYE MATENDO KILE UNACHOAMINI KUHUSU MUNGU KWA JAMII YAKO. Hivyo zipo faida ambazo binti anazipata ikiwa atajua kuwa upo umuhimu wa kumtumikia Mungu akiwa bado kijana ambae hajafungwa na nira ya ndoa.
So kumtumikia Mungu ukiwa bado binti NI MCHAKATO AMBAO UNA MAENEO KADHA NA NINGEPENDA KUANZA na eneo la kwanza:
1.HUWEZI KUMTUMIKIA MUNGU USIYEMJUA UKAMFAIDI KWA ASILIMIA 100. Swali,Je unamjua Mungu kwqa kiwango gani? Je unafahamu nini maana ya KUMJUA MUNGU
Changamoto zote unazokutana nazo zinaweza kukumeza au la kwa kutegemea KIWANGO CHAKO CHA KUMJUA MUNGU...
Kumjua Mungu kunakufanya UFIKE UKOMO WA KUKARIRI NA KUONEWA,Kumjua Mungu ni kufahamu mengi kuhusu Mungu na la kwanza ni hilo kwamba yeye ndiye Mungu aliyekuumba yaani mahusiano yako na yake...Unapomfahamu baba yako mzazi KUNA HALI YA UTULIVU UNAIPATA NDANI YAKO inayokupa picha ya KUFIKIA MWISHO WA MATESO YAKO hata kama baba yako hana uwezo..
Nimesema eneo la kwanza katika safari yako ya kumtumikia Mungu kama binti ni KUMJUA MUNGU...Mhubiri 12:1 inasemaje?
MKUMBUKE MUUMBA WAKO SIKU ZA UJANA WAKO....ukweli ni kwamba huwezi KUMKUMBUKA kama HUMJUI...huwezi kumkumbuka kama HUWA NA MAHUSIANO NAE...huwezi kumkumbuka kama huna SABABU YA KUMKUMBUKA....huwezi kumkumbuka kama HAJUFUNGULIWA UFAHAMU ujue amekufanyia mangapi ili upate akili.
Hilo neno KUMKUMBUKA ni zaidi ya tafsiri ya neno REMEMBER..
kwa mfano wengine mko hapa mnawakumbuka akina alehandro wenu wa zamani, hahah haha si eti eee?
Wengine mnakumbuka ugumu wa maisha yenu
wengine mnakumbuka wazazi wenu kwa mambo mazuri au mabaya
narudia tena...Neno KUMBUKA ni zaidi ya REMEMBER au MEMORY...na ukitaka ujue maana yake halisi ni lazima ujiulize swali moja kubwa...KWANINI UNAKUMBUKA au NINI KILITOKEA MPAKA UKUMBUKE...maana ya MKUMBUKE MUUMBA WAKO ni ISHI UKIJUA...ISHI UKIZINGATIA..ISHI UKITAMBUA...kuwa UMEUMBWA NA ALIYEKUUMBA YUPO NA NDIYO ANAITWA MUNGU-MUUMBA WAKO...tuko wote?
Ndani neno KUMBUKA kuna mambo ya msingi sana ya kujua wewe kama binti.Unapokumbuka kuna mambo utayaona na napenda niwatajie tu kwa sasa....Kila unapokumbuka utaona:
1.Sababu ya kukumbuka,yaani utaona nini kilitokea ambacho kikagusa maisha yako kwa uzuri au ubaya kwa kiwango ambacho mtu huyo akaingia moyoni mwako na mpaka sasa unapokumbuka picha ya lile jambo inakuja waziwazi kwako....KUMBE KILA KUMBUKA INA SABABU NYUMA YAKE...oooh haleluyaaaaa najisikia kupaa hapa hahahahah
2. LOCATION,kila unapomkumbuka Mungu utaona ile sababu ilitokea mahali fulani, hata kwenye maisha ya kawaida pia utaona ile sababu iliyosababisha mambo kutokea ilitokea mahali fulani na ndo maana kuna wengine mpaka leo mnaogopa GIZA kwani kuna mengi yalitokea gizani...wengine hamtaki kupita mitaa fulani maana inawakumbusha vitu fulani....JE UNAKUMBUKA ULIKUTANA WAPI NA MUNGU MPAKA LEO UMKUMBUKE BKOZ UNAMJUA?
3. PEOPLE,unapokumbuka pia utawaona watu,ndio watu waliohusikia na kukusaidia kumjua Mungu,
4.MUDA, yaani yote hayo yalitokea kwa majira yake na nyakati zake
so turudie tena Mhubiri 12:1 inasema......?
So nikuulize kwa kuangalia hayo maeneo manne unaweza kusema nini kuhusu wewe na kama unamjua Mungu?
Unaona uhusiano wa Kumjua Mungu na namna ambavyo Mungu amekufunulia kwa njia mbali mbali mamabo kadhaa ambayo kwa hayo unasema unamjua Mungu
So unaposema unamjua Mungu maana yake kuna tabia za Mungu umezijua na zitaonekana ndani yako wewe kama binti...kuna FIKRA ZA MUNGU zitakuwa ndani yako...lazima utakuwa na SHUHUDA za namna ambayo Mungu kwa kutumia yale mambo manne ya KUKUMBUKA alikusaidia kumjua kwa namna moja au nyingine...
Hiyo pia ina maanisha kuwa UKIMJUA MUNGU utakuwa na maisha ya NIDHAMU kwani unafika mahali unatambua kuwa IPO MAMLAKA kubwa zaidi kuliko wewe ambayo ndiyo iliyokuumba na hilo jambo unatakiwa uishi ukijua kila siku na kila mahali...ukisahau tu ujue unatengeneza mazingira ya kujiharibu...hata ukiwa chooni usisahau kuwa MUNGU ANAYO MAMLAKA JUU YAKO na ndiye aliyeekuumba utaona jinsi maisha yako yatakavyobadilika na kuwa MAISHA YA IBADA...
Kumbuka kila ktu kinachofuata au ambacho ungependa kukifanya katika maisha yako NINATEGMEA SANA NI KWA KIWANGO GANI UNAMJUA MUNGU...yaaani MSINGI wa kila kitu katika maisha yako kama binti ni KUMJUA MUNGU...ukimjua Mungu unapata uchaji na kuishi maisha ya KUMCHA MUNGU na hapo ndipo unakuwa unaishi na HOFU YA MUNGU maana umetambua ukuu wa Mungu katika maisha yako....
Ukijikagua kwa mambo ya point hii ya kwanza unapata nini katika maisha yako? Unaona ni maeneno gani umekwama? Je umemtumikia Mungu au unamtumikia Mungu kweli? Je unamkumbuka Muumba wako ukiwa bado binti? Je una visingizio? Na kama kuna mambo yaliyopita yanayokuumiza mpaka sasa basi ACHILIA,SAMEHE,JISAHEME na UJIKUBALI kama unataka kusonga mbele. Unaruhusiwa kunifuata INBOX kama unaona tunahitaji kufanya zaidi ya kuzungumza hapa maana huu ndio wakati sahihi.
By Pastor Raphael JL:
0767033300.
Hakuna maoni: