Ads Top

WHOEVER CAN MOVE GOD, CAN MOVE ME.


Ukiri Wangu:Nakataa kupangiwa uwezo na mwanadamu. Uwezo wangu ni Zaidi ya cheti cha kidato cha nne, au cha sita au cha chuo kikuu. Uwezo wangu ni Zaidi ya kupata alama A kwenye mtihani. Uwezo wangu ni kusudi langu. Uwezo wangu umefichwa ndani sana kama kuitafuta tanzanite chini ya ardhi. Na ndio maana, nakataa kukata tamaa kwa kufeli mtihani darasani. Nakataa kukatishwa tamaa kwa kutofikia kiwango kilichopangwa. Nakataa kujiona sifai eti kisa nimefeli mtihani. Nakataa kujiona siwezi eti kisa nimeshindwa mara moja. Nitawajibika. Kila nililofanya na kupatia ni ishara kwamba ninayo mengi ya kupatia ambayo bado sijayafanya. Kila nililofanya na kukosea ni ishara kwamba huenda nafanya kisicho changu, huenda nimezembea au kuna nisilolijua. Nakataa uzembe. Kuanzia sasa, nitaongozwa na kile ninachoamini. WHOEVER CAN MOVE GOD, CAN MOVE ME.

Pastor Raphael JL:
0767033300
DODOMA.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.