CLOSET PRAYERS TESTIMONIES (From 18th-19th August 36Hrs)
36
HOURS CLOSET PRAYER
AUGUST
18-20TH 2017
THEME:
REPOSITIONING YOURSELF
TESTIMONIES
ROSEMARY
Namshukuru Mungu sana
kupitia mtumishi wake na nyie wote humu
mmenifanya nione umuhimu wa kumrudia Mungu. Nina amani sana rohoni
mwangu.Namuomba Mungu anisimamie katika safari yangu hii mpya ya kumtegemea
yeye tu. Asante Mungu kwa kuniokoa mimi mdhambi. Asante sana dad kwa upendo
wako na uongozi wako mpaka mimi mwenyewe kwa hiari yangu nimeamua kuokoka.
Mungu atubariki sote na atuongoze.
GRACE MAPHIE
Namshukuru Mungu kwa maombi ya jana nimemwona
hakika pia naendelea kujifunza Daddy ubarikiwe.
Naendelea na maombi ya kurudi
kwenye nafasi lakini namshangaa huyu Mungu jana nimeweza kufanya jambo ambalo
hapo nyuma nilikuwa nafanya kwa kusuasua yaani jana sio kwa huo upenyo niliouona
nalibariki jina la Mungu wetu
HILALIA PHILIPO
Jana wakati naingia kwenye maombi
ya Toba ni kama nililetewa CD ya maisha yangu ya mwanzo NILIPOANZA WOKOVU. Nikawa
naona nilivyokuwa MOTO WA KUOTEA MBALI. Nikakumbushwa mambo mengi ambayo
nilijikuta mimi JINGA KABISAAAA NILIIKUWA NIMEKUBUHU. NIKAOMBA MUNGU ANISAMEHE.
DAH until NOW bado naona ule mda wa Toba hautoshi aisee. Yaan naona nilipotoka
kwenye nafasi yangu yaani kama nilipanga nafasi ambayo iko mbali. Kurudi
inahitaji GHARAMA KABISA. Na nashukuru
MUNGU kadri navyoendelea kuomba Toba ndo kadri navyoendelea KUPATA AMANI ZAIDI. Yaani natamani tuendelee mpaka
SIKU YA UNYAKUO AISE.
Nawaza mambo mengi mpaka NAKOSA
NENO LA KUMPA MUNGU KAMA SHUKRANI NA KUNIPA UFAHAMU HUU AMBAO HATA MAKANISANI
KWETU SIJAWAHI KUSIKIA.
Aisee. Kwanza hata style ya
maombi imebadilika. Kuna wakati nilikuwa nikiomba yaan hata sielewi nimesema
nn. Dah yaan i dont know how to say to God. Am SPEECHLESS
QUEEN FLETCHER
Namshukuru sana Mungu kwaajili ya
jion hii...Kila Mara nikiona shuhuda mbali mbali I was wondering mimi mbona
sielewi elewi bado... Well Mungu amenifungua. Amenifunulia majibu jion hii. Amenionyesha
how much wrong I was in my life and live out of my position for so Long. Thinking
that I was right...Roho mtakatifu kanichimbua yale yaliofichika.
Nimejikuta nacompare with what
dad was teaching us nikawa nalia tu.In short I was thinking the way Am living
is right and that how it's supposed to be... lkn baada ya kufunguliwa nimejiurumia
mimi. Namshukuru sana Mungu anaeendeleakunifanya mpya. I feel so good now. Namuomba
Mungu akamilishe kaz aliyoianza. I want the whole package in Jesus name
Yaan NANG'ANG'ANA!
God is good
This is my Testimony.
ELIZABETH KING
Ngoje niseme ukweli tu, hivi
unajua ninaomba kwa raha sana situmii nguvu wala sijikakamui wapendwa, unajua
maana navyokaguliwa na kukumbushwa mahali nilipoangunga, na natubu ilo eneo
nalokumbusha najihic mwepesi sana, halafu naomba kwa utulivu wa hali ya juu, mtaa
huu unakelele but si kwa utulivu huu
nilioupata, jamani si kwampangilio huu wa hoja zenye nguvu hadi nakaa najiuliza
hii aina ya maombi ya namna hii ni mimi naomba au jamani dah nashindwa kuelezea
wapendwa...
Unajua nini huku kutoka kwenye
nafasi kulinifanya mpaka nikiwa nataka kusoma neno la Mungu moyo unanipasuka
wapendwa yaan kama nimekutana na el- shababu, yaan mwanzo nilitamani hata
kutofanya haya maombi, coz nilikuwa naona kila kitu baba alichoongea kama ndo
kinanivuruga zaidi, nikawa nasema hivi mbona hali kwangu ni mbaya saana na ndo
kwanza giza linazidi kutatanda...
Yaan nimekaa hvy hvy kwenye group
kishingo upande huku nikijiandaa kuingia kwenye maombi ya jujikakamua, na mara
nyingine hata uelewi unachoomba, miayo mingi yaan fujo tu.... ila jamani mwacheni
Mungu aitwe Mungu cku moja kabla baba ajasema anataka kuwapunguza watu
wasiochangia nikaanza kupitia somo ili alilofundisha taratibu, sasa ndo
nikalipenda na nikapata hamu ya dhati kutoka moyoni kulifuatilia na ndo mwanzo
wa mimi kuanza kuelewa yaan kupata ufahamu wa hiki alichotufundisha....
Jamani nikisema kurejeshwa kwenye
nafasi, kutakaswa, kufunguliwa fahamu, kutulia madhabahuni kwa Bwana, na kusoma
neno na ukawa unalielewa raha, jamani na maanisha nachosema, ni maombi yangu ya
mara ya kwanza kabisa kuona Mungu anajibu maombi kwa haraka namna hii, kweli c
kila neno linalosema nakuaminiwa na watu wengi lakuliamini jamani Mungu ajibu
maombi mpaka badae kesho tu nk, lkn Mungu anajibu maombi hata wakati huo
huo, Mungu ni mwema kwangu jmn...
JUSTINE YOMBO
Bwana Yesu asifiwe wapendwa,
namshukuru Mungu kwa kuniunganisha na mtumishi wa Mungu @RaphaelJL, kupitia
maombi haya nimeuona mkono wa Bwana. Najisikia wepesi ila Mungu amefanya zaidi
ya hapo. Baba ulisema Jumatatu tukafanye kazi mimi ntaenda kufanya kazi Jumatatu.
Wapendwa ukiwa nje ya nafasi yako baraka zako haziwezi kukulocate. Kila kitu
kinacho kuhusu kipo kwenye nafasi yako. Sina mengi zaidi. Namshukuru Mungu kwa
progress hii. Haya maombi ni mpango wa Mungu kuturejesha mahali sahihi.
AMINA MNZAVA
Nina ushuhuda mkubwa Mimi
nimepona jamani uwiii, nilikuwa natengeneza Na mpenzi wangu nilinunua La plot
na nikaanza kujenga bila kumwambia, nimetengeneza jamani maana mahali
tulipokuwa tumefika khaaa pa bays asante Mungu kwa kuijua nafasi yangu
kama.msaidizi nimerudi mwanampotevu. Tumepona ndoa yangu imepona Jina lake
libarikiwe
GRACE MAPHIE
Namshukuru Mungu kwa neema na
rehema zake hakika nimemwona kwa namna ya ajabu we Mungu ni mkuu hakuna aliye
kama wewe matendo yako bhana siwez kueleza.
MRS. CELINA MAGIGITA
TWEKA MPAKA KILINDINI. SAMAKA
WAPO, ISSUE NI KUSIKIA BWANA ANASEMA NINI...TWEKA MPAKA KILINDINI
4 Hata alipokwisha kunena,
alimwambia Simoni, Tweka mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki.
6 Basi, walipofanya hivyo
walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika; (Luka 5 :4, 6)
Shalom wana wa mfalme!
Ninarejea msisitizo wa Mchg. Tweka mpaka kilindini!
NILICHOSIKIA KWA BWANA MASAA YA
MWISHO KATIKA KUHITIMISHA MAOMBI YA KURUDISHWA KWENYE NAFASI.
HISTORIA YANGU YA UFUGAJI.
2008 nilianza rasmi ufugaji
nikiwa nafugia nyumbani kwangu. 2010 Bwana alipanua hozi yangu nikajieneza na
kupata shamba Miyuji, nikajenga mabanda makubwa ya kutosha kuku 2,000 kwa mara
moja. Nikahamishia mradi huko baada ya kujenga kiwanda kidogo cha chakula cha
mifugo na nyumba ya watenda kazi. Nikaweka kuku 2,000 hali ikawa nzuri sana kwa
wiki nikawa nauza tray za mayai 400 Kibaigwa na soko kuu la majengo kwa wauzaji
wadogowadogo. Ibilisi hachezi mbali aliingia kupitia mtoto wa wifi yangu
akaniibia sana nikaishia kuufunga huo mradi mwaka 2015.
Dec 2016 mume wangu akanitia moyo
nikainuka tena nikaanza kufuga nikaweka kuku wa nyama (chotara) 1,000. Wakaenda vizuri kwa muda mwezi
Februari ghafla mdondo ukawaingia wakafa kuku 600 ndani ya wiki moja. Tangu wakati
huo nilikata tamaa kabisa kufuga nikaplan kubadili matumizi ya hayo mabanda kwa
kuwa wiki ijayo nitaanza mradi mpya wa kukoboa,
kusaga na kupaki sembe nikawa nimepanga nitayageuza yawe maghala ya
kuhifadhia mahindi.
Usiku nimemuomba Bwana aseme nami
neno katika kuhitimisha maombi, nikautuliza moyo wangu kwa Bwana pasipo kuwazia
kabisa ishu ya miradi wala biashara maana nilishafikia maamuzi ya kufanya sembe
na duka la mavazi tu, hivyo hilo eneo la kazi za mikono sikuwa na mzigo wa
kuliombea kabisa kwenye hizi siku 3 in fact sijagusa kabisa kuombea biashara,
siku zote nimekomaa na matengenezo na kurudishwa kwenye nafasi tu.
NILICHOSEMESHWA KWA NDOTO!
Usiku wa leo mida ya alfajiri ya
saa 10 nimeota ndoto hii.
Nimeona katika ndoto niko
natembelea mradi wa kuku wa nyama na mayai wa mama 1 ana kuku wengi sana.
Nikamwambia nimekuja unielekeze mtu sahihi wa kuniuzia vifaranga ili nikafuge.
Akanitajia wauzaji 2 mmoja ni mtumishi Pallangyo nikamwambia nitachukua kwa
Mtumishi Pallangyo kwa kuwa ninamfahamu.Nikastuka ndotoni.
NASISITIZA HATA KUWAZA TU KUKU
SIJAWAHI KUWAZIA!
Binafsi nimemshangaa sana Mungu.
Huu ni urejesho wa aina yake naiona Zaburi 126: 1 imekuwa halisi kwa hiki cha
leo!
"Bwana alipowarejeza mateka
wa Sayuni, Tulikuwa kama waotao ndoto". (Zaburi 126 :1)
Ninamshangilia na kumfurahia
Bwana kwa matendo makuu aliyonitendea kupitia hii programu.
MUSA JOSEPH
Kipekee namshukuru sana Mungu
kwanza uombaji ni lazima ubadilike...Ukipata ufahamu kuomba kuna badilika sana
jamani.
IMEKUWA DHAHIRI KWAMBA MUNGU
AMENIREHEMU NA AMENIFUNGULIA MILANGO AMBAYO HAKUNA AWEZAE KUIFUNGA.
Barikiwa Dady.. Ninakupenda sana.
MUNGU WA MBINGUNI APOKEE SIFA
ZOTE NA UTUKUFU.. HAKIKA AMEFANYA JAMBO
KATIKA MAISHA YANGU.
Semina ya jana... Na leo pia ninaendelea
kupata mkazo wa Waefeso 6:10-18
MUNGU NA ANISAIDIE KATIKA
KUUTENGENEZA UFAHAMU WANGU...
ESTER WILLIAM
Kwakweli Mi namshukuru Mungu ktk
maombi haya, kwanza kabisa shetani alikuwa amejiinua kwangu kuhakikisha
sifungi,ijumaa nimeamka kidole cha mkono kinaniuma sana kilikuwa kimeanza kidogodogo
kuvimba nikaamka kimezidi sana nikaenda hospitali wakakipasua nikarudi na
maumivu makali nilipewa na dawa za kumeza, nilichofanya nikasema hapa sinywi
dawa yoyote hadi jumapili, ndo takunywa, nilishauriwa na nispo kunywa dawa
kitaoza nikajibu dawa nitakunywa ila jumapili, nilichekwa na kuambiwa nyie
walokile mnakazi kwani Mungu hajui kuwa unaumwa? ila nashukuru ndivyo ilivo
kuwa.
Nashukuru najiona nina badiliko
kubwa ndani yangu, hasa likutamani niongee na Mungu kila saa, nipo tofauti na
nilivyokuwa,Mungu akubariki saana Pastor kwa maono haya umetupa kusimama ktk
nafasi tulizotakiwa tuwepo.
Jana napo shetani kainua vita juu
yangu, kuna binti wa kazi, nilikuwa nimebaki nae,ana umri wa miaka17, ilikuwa
yupo karibu kuondoka kwao anakaa dodoma kuna baadhi ya hela yake alikuwa anaisubiria,
nikamwagiza mboga mda wa saa 4 asubuhi, kaenda jumla hajarudi hadi sasa, ila
najua hiyo itakuwa ni roho chafu iliyopo katika hii nyumba, maana historia
iliyopo ndiyo hiyo zaidi ya mabinti wa4, wanaondoka kwa stahili hiyo, nitahakikisha
nasimama katika nafasi yangu kuiteketeza hii roho, nakuhakikisha kujua huyu
bint alipotorokea na arudi aje aondoke kwa amani, nimekuja tu mara moja dar kwa
mama wa hiyari ndo yanatokea baya naamini Mungu amenileta kwa makusudi mahali
hapa lipo kusudi lake huruhusu yatokee haya.
MUSA JOSEPH
Esfeso 6:10-18
10 Hatimaye, mzidi kuwa hodari
katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.
11 Vaeni silaha zote za Mungu,
mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
12 Kwa maana kushindana kwetu
sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa
giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha
zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza
yote, kusimama.
14 Basi simameni, hali mmejifunga
kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,
15 na kufungiwa miguu utayari
tupatao kwa Injili ya amani;
16 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya
imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.
17 Tena ipokeeni chapeo ya
wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;
18 kwa sala zote na maombi
mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika
kuwaombea watakatifu wote;
Katika mlolongo huo maombi huwa
ni ya mwisho. Cha kwanza ni silaha ambazo zitapatikana kutokana na ufahamu
sahihi.
Kupingana na hila za shetani ni
zaidi ya maombi ni lazima kwanza uwe na ufahamu wa silaha zote.
Kuna watu wanaomba sana na
hawapat majibu ya maombi yao.
Kwanza ni lazima kuwa na ufahamu
sahihi wa kitu gani unakiombea..
Mungu anayejibu maombi huangalia
usahihi wa maombi na sio wingi wa maombi na kinachofanya maombi yajibiwe ni
kiwango cha nguvu kilicho ndani yako.
Ili uombe maombi ya muda mrefu
kwanza unahitaji ufahamu sahihi then nguvu ndani yako.
Ni kitu kibaya kuwa na ufahamu
usio sahihi na kwenda mbele za Mungu.
Maana yatakuwa ni maombi ya
mpumbavu..
Ukizielewa silaha zote zilivyo
hapo ndipo hata maombi yataenda sawa.
Uhodari katika Bwana hauji kwenye
maombi, uhodari unatengenezwa kwenye mchakato... So ninlazima kuwa na ufahamu
sahihi wa Neno la Mungu.
Shetani ni tofaut na mapepo,
hakemewi akatoka yeye ni mkuu wa nguvu zote za giza..yeye tu ndo anauwezo wa
kutokea mbinguni.... Shetani anatolewa kwa ufahamu sahihi.
Ufahamu ndio unaomkemea shetani..
Kama hujui kweli kwenye eneo husika huwezi toka.
Mathayo 4:1---
Yesu alikuwa na ufahamu na ndo
maana alimshinda ibilisi.
Usiingie kwenye maombi kama
hujavaa silaha zote...
FRANK MTAHA
Kibinafsi namuona Mungu sana
katika mambo mengi mno.
Kwanza nimekuwa mwepesi sana wa
kuomba kwa kiwango kikubwa, pili amani ya ndani imeongezeka maradufu na kuna
mambo aambayo nalikuwa na hofu nayo kwamba sitafanikiwa lkn sasa hivi moyoni mwangu
ninasema HAKUNA JAMBO GUMU MBELE ZA MUNGU, tayari nimefanikiwa moja tena katika
kusema tu kwamba hii ni milki yangu na kweli imekuwa.
Kwenye huduma leo ndipo Mungu
alipojidhihirisha kabisa ubaarikiwe pastor kwa somo hili na utaratibu mzuri wa
maombi ulioongozwa na Roho wa Bwana,Mungu ni mwema sanaa
SAINA KITTA
Jaman nashindwa hata nisemaje
maana nimemuona mungu kanifungua kabisa , mpaka najiona mwepesi mungu azidi
kukupa maono mtumishi wa Mungu
AMINA MNZAVA
Jamani ni shuhuda kwa kweli
nilipoamka asubuhi nikiwa nimekaa nikapata wazo la kuanzisha huduma ya wanawake
inaitwa WOMAN of GLORY, sijawahi kuwaza hii heading naamini Bwana aliyeanzisha
kazi hii ataikamikisha utukufu kwa Mungu.
CONCESA SHUBIRA
God's mercy has been shown unto
me during this prayer season. Finding my position and being re-stablished in
Him through the prayers and actions has brought me nearer to the Lord. This
journey has been a revealing one for me. Meditating upon the word each day and
learning that there is more in my life that God has planned for me, and not only what i know. I can brag and say
that Jesus has done it again!!!
He is a wonderful and merciful
God.
Thank you daddy for this sesion
am grateful to have you.
Stay blessed everyone!!
DOREEN KIARRA
Maombi haya hakika hayakuwa ya
kawaida. I am tooo blessed... , na shuhuda zazidi kunibariki pia. Mungu wetu asikia na ajibu. And He moves
instantly
MRS. CELINA MAGIGITA
USHUHUDA WANGU
Utangulizi:-
Mnamo Tarehe 10/08/2017
nilijiunga rasmi ndani ya hii Safina. Kupitia rafiki yangu mpenzi Mrs Amina
Myombo.
Nikajitambulisha hivi:-
Mrs Celina Magigita. Nimeokoka,
mfanyabiashara, kihuduma ni mwalimu na mhubiri, ninaishi Dodoma. Nipo humu kwa
nia ya kuvuka nilipokwama. Asanteni kwa ushirikiano. Nimesoma masomo kupitia
dada Amina, nimebarikiwa sana. Tupo
pamoja ndugu katika Kristo Yesu.
Shauku na Nia yangu kuu kujiunga
humu ilikuwa KUVUKA NILIPOKWAMA!.
Neno linasema:-
"Nawe utakusudia neno, nalo
litathibitika kwako; Na mwanga utaziangazia njia zako". (Ayubu 22 :28)
Kusudi langu halikuwa kuja
kufahamiana na watu au kushangaa bali nilikusudia KUVUKA. nilimaanisha
nilichokusudia na nikadhamiria KUVUKA.
Leo hii ikiwa siku 10 ndani ya
SAFINA ninazo shuhuda kuu 3 za matendo makuu ya Mungu naam na ya 4 iko njiani
naitarajia kuipokea wakati wowote ambayo ndiyo muhimu zaidi kwangu.
Mambo niliyotendewa ni:-
1. Akili zangu zimefunguliwa
nimeelewa ili kuishi maisha ya Ushindi jambo kuu ni kuwa na UFAHAMU sahihi wa
hilo eneo. Kwa hiyo nimejipanga kulipa gharama kujaza moyo wangu maarifa ya
kiungu ili nipate ufahamu wa kutosha kuishi maisha ya utoshelevu na ushindi
huku nikilitumikia shauri la Bwana.
2. Asante Ujinga imeniondoka,
nimetembea kwenye mateso ya kujitakia ndani ya ndoa yangu kwa zaidi ya miaka
17. Kupitia maarifa niliyoyapata humu nimeweza kufanya maamuzi magumu ya kukaa
kikao cha masaa 3 na kuwekana sawa na mume wangu hatimaye tumerejea Eden. Hali
haikuwa nzuri kama ni shimo basi adui alishaliweka tayari kunitumbukiza. Asante
mchg. Raphael kwa kunivusha nisitumbukie.
3. Eneo la uchumi limekuwa na
mapito mengi sana na sintofahamu za hapa na pale. Kwa neno la mwisho alilonipa
Bwana kwa njia ya ndoto nilipokuwa nahitimisha maombi. Limetosha kunipa kujua
BWANA ananirejeshea utukufu wa NAFASI yangu kiuchumi.
4. Eneo la Kiroho hili ni nyeti
zaidi kwangu na sijaelewa kwa nini Mungu amelifanya kuwa la mwisho kukamilishwa
muujiza wake!
Nimekuwa katika mapito magumu
sana yaliyopelekea mahangaiko ya kutokuwa na mchungaji mmoja wa kunilea kiroho
kwa muda mrefu na shida kubwa ilikuwa baba wa familia kutaka nibaki kwenye dini
nami nang'ang'ana kutaka kumtafuta Mungu kiroho zaidi badala ya kujifungia
kwenye kifungo cha dini na mapokeo ya dhehebu.
Juzi kwenye toba na matengenezo
nilikaa na mume wangu nikafanikiwa kujieleza kwa msaada wa Roho Mtakatifu
hatimaye amenielewa na kukubaliana na ombi langu la mimi kupewa uhuru wa mahali
pa kuabudu kiroho.
Huu kwangu ni muujiza mkubwa sana
lakini haujakamilika bado ndio kwanza nimeanza kuomba Mungu anipe mchungaji
sahihi wa kunilea kiroho ikiwa ni pamoja na huduma na utumishi uliomo ndani
yangu.
Bwana ameahidi,
"nami nitawapa ninyi
wachungaji wanipendezao moyo wangu, watakaowalisha kwa maarifa na fahamu"
(Yeremia 3 :15)
Suala si kuwa ndani ya kanisa
maarufu, jengo zuri nk.... Muhimu kwangu ni ninalishwa nini na hicho
ninacholishwa kinanipa maarifa na ufahamu wa kutosha kuishi maisha ya
utoshelevu pande zote na yanayompendeza Mungu!
Kwa huyu mtoto wa 4 ni muujiza
ambao haujakamilika nawiwa kusema haya kwa pst Raphael.
Petro alitekewa alipokuwa uweponi
mwa Bwana akaishia kusema na tujenge vibanda vitatu.. ...nahisi kuna mambo
aliona bado hayajapatiwa majibu akatamani waendelee kubaki mahali pale kwa muda
zaidi ili apokee yote kwa ukamilifu wote.
OMBI LANGU.
Humu ndani sijui kama wote
tumevuka kwa kuzaa vile tulivyoingia nanvyo ndani ya Safina na tumetosheka kwa
vile tulivyofanikiwa kupush hata tukazaa.
Binafsi mtoto namba 4 hajazaliwa
mkamilifu ni premature anahitaji kusaidiwa ili akamilika na leo ndio mwisho wa
hii incubator nawaza peke yangu joto nililo nalo litatoshea kumkamilisha! Bado
sijaliamini joto langu hivyo ninaomba extension ya muda atakaona unafaa mbeba
maono pst Raphael ili mtoto huyu akamilishwe na kukamilisha ushuhuda huu muhimu
kwangu kiroho.
Naomba hekima yako mtu wa Mungu
na muongozo ikiwa nitapata kibali moyoni kwako.
Jambo moja ninajua hakuna mtu
anayefanikiwa pasipo msaada wa watu wengine. Kwa hilo nilijifunza
nimejifunza kunyenyekea na kuheshimu
mchango wa watu kwenye hatma yangu.
Mchg. Raphael umeongeza thamani
yangu kwa kuniweka kwenye njia sahihi kuielekea hatma yangu ya utukufu. Ni
maombi yangu Mungu akuinulie watu wakuu watakaokushika mkono na kuongeza
thamani ya maisha yako hata uufikie ukamilifu wa hatma yako duniani.
Nawapenda katika wote Bwana.
Mmefanyika baraka kwangu kwa hizi siku 10, niliomba ushirikiano nilipoingia
humu, namshukuru sana Mungu kwa ajili yenu kwani mmenipa ushirikiano mkubwa na
kunirahisishia kupokea kwa kasi ya ajabu.
Barikiweni,
Celina.
IRENE JORAM
Namshukuru Mungu kwa haya maombi,
na kwa ufahamu niliopokea kuhusu Nafasi yangu na jinsi ya Kusimama.
Binafsi, nmekua nikipitia katika
kipindi cha kutamani kuyarudia matendo ya kwanza na kumuomba Mungu arejeze
furaha ya wokovu na kumtumikia katika nafasi aliyonipa. So, imekua ni process
ilikua tayari nimeanza, nilipoona title tu ya prayers nikajua Mungu ana jambo
anataka kufanya katika maisha yangu. Nmashukuru amerejesha furaha na shauku
niliyokuwa nayo mwanzo ya kumtafuta na kumtegemea katika kila jambo.
Amerejesha shauku yangu ya
kuandika pia ambayo ilianza kupotea, hata tu kuandika notes za haya masomo bila
kughaili kwangu ni ushuhuda mana nilikua nimeshafika pabaya. Katika yote nazidi
kujifunza kuwa mtii na kufanya yale yanipasayo kufanya Kama mwana.
Baba nakushukuru kwakua hujawahi
choka kunilea na kunionesha njia sahihi, kila ninapopitia changamoto hujachoka
kunishauri na kuniombea. Mungu akujaze pale ulipopunguza na akuhuishe maradufu.
All Glory to God in the highest!!
ESTHER MWAIJANDE
Ubarikiwe sana baba yangu. Nakosa
hata maneno ya kuongea, naishia kusema UTUKUFU KWA MUNGU. Daddy umetumika kuyabadilisha
maisha yangu kwa kiwango kikubwa sana maana nilipokuwa nimefikia ilikuwa ni
kiuangamia tu. MUNGU NINALITUKUZA JINA LAKO.
HILALIA PHILIPO
Mungu ni mwema nashukuru Mungu
kwa kunitia nguvu. Kuna jambo ambalo nilitaman kulianza mda mrefu sana lakin sikuwa
na hamasa ndani yangu kulifanya lakini baada ya kuanza maombi haya na kumuomba
Mungu anirejeshe katika nafasi yangu katika suala zima la KUTUMIKA nikajikuta ninapata nguvu ya ajabu na hamasa
Moyoni mwangu kuanza upya na kuendeleza plans ya jambo nililokuwa nataka
kufanya.
Na pia napenda kumshukuru Mungu
naona mabadiliko katika suala zima la MAOMBI. Nimeona ni namna gani MUNGU
kanitengenezea utulivu flan amaizing katika maombi na kuwa na shauku ya
kuendelea kuomba.
Pia katika suala zima la kujifunza.
Hili suala la NAFASI lilikuwa jambo jipya na limenifanya nikakumbuka WOKOVU
niliokuwa nao wakati nauanza na kujigundua asilimia 200% nilikuwa nilishapotea
na kutoka katika wokovu huo. Yaan hata nguvu niliyokuwa nayo ilikuwa hakuna
hata chembe. Ilikuwa like am forcing myself. But now i see GOD ANANITENGENEZA UNTIL NOW. YAAN HAPA
NIMETEKEWA KABISAA NA NGUVU ZA BWANA WA MAJESHI.
Dady Mungu aendele KUKUMIMINIA
MIBARAKA na Mungu akupe haja za moyo wako.
Nakupenda baba.
DESTEA KAGINE
Mungu akubariki na akuinue kwa
viwango vya juu zaidi Pastor Raphael. Kwa hakika huduma yako ni njema sana.
Binafsi nimemwona Mungu sana kupitia maombi haya.
ELIZABETH KING
Hahahahah…….nianze
hv tu, kwasababu siunajua kila kitu ulichokiwa unatamani kukipata sikunyingi
sasa umekipata eee, so lazima uwe unacheka, unajua nikisema Mungu wetu ni mzuri
kila mara nasema nikiwa na cheka bafuraha isiyo kifani si kwaaajili yangu tu
bali na kwaajili yenu, MUNGU WETU AMETUKUMBUKA WAPENDWA,
1. Namshukuru Mungu mno kwakunipa
ufahamu, maarifa, hekima, nimerejea kwenye nafasi, unajua kuna neno linasema
walio wa Mungu, Mungu anawajua.. Hapo nilitaka kusema Baba umjua mwana, na
mwana umjua Baba, sasa hivi nikisema mimi ni mwana wa Mungu sisemi kwa mashaka
tena naamini hivyo na Baba anajua hivyo kuwa mimi ni mwanae, so baada ya kupata
huo ufahamu, sasa sigombanii tena nafasi kwa Baba, nilikuwa na shida ya pesa
kiasi fulani na nikawaza nitapata wapi, nilipo lifikisha ilo swala kwa mama,
mama angu anatabia ya kuniuliza ya kazi gani, lakini ilo swali jana sikusikia
nilitaja kiasi na nikapewa na zaidi, nambariki Mungu juu ya hili.
2. Nilikuwa niko vizuri mno
najirani yangu ghafla akaanza nipita bila salamu ananipandisha ananishusha,
nikasema moyoni huyu mdogo kwangu nitamwonesha kama mimi ni zaidi yake,
nikajitenga mbali nae sasa tunaanza maombi nikakumbushwa kupatana na mtu alie
nikosea ikabidi niende kuongea naye, nimuulize kulikoni mpendwa basi akanieleza
yote nilio mkosea hadi kufikia hatua hiyo, na yote alinihisi tu haikuwa kweli
kasoro moja ndo lilikuwa kweli, tukaombana msamaha tukapatana sasa hivi mambo
ni shwari.
3. Nashukuru pia kwa maombi haya
kwasababu yamenipa majibu mengi saana ya maswali niliokuwa kuwa nayo mengi ya kiroho
na kimwili niliokosaga majibu kwa muda mrefu, kupitia maombi haya nimepata
majibu yake, namrudishia sifa na utukufu Mungu.
Asante pia Pastor Raphael, wewe
ni mtumishi wa Mungu ulonisaidia mno upande wa kiroho, Mungu akubariki saana
wewe na familia yako, na aendelee kukuzidishia mara dufu, atimimize kusudi la
huduma hii, uendelee kufanyika baraka na kwa wengine wengi... simalizi jamani
Mungu akubariki mno.
REBECCA AMOS
Shalom jaman,, kwa majina kamili
Naitwa Rebeca, nimepata fursa ya kuwa humu kwa kipindi chote.... niliingia humu
kwa sababu ya title ya tangazo reposition nmetamani sana kwa kipindi kirefu
kuirudia nafasi yangu kimungu ila nilikuwa nakosa pa kuanzia ..... nlipoteza
taste ya maombi..... yaani safar yangu was vuru vuru, watu wa Mungu nlikua na
muda finyu lakini kila nkikumbuka kua nataka kurudi kwa position yangu ilinipa
hamu na hatua maana nliona hii kama nafas ya pekee,, toka ijumaa sa ni kama
nimelishwa pilipili yaan duh ni haielezek kwanza amani ya moyo nliyonayo pili
naona kama nimeokoka jana serious nimepata zaidi ya nlichotarajia maana nimekua
connected than ever before. Nina furaha na raha,, nlishasahau kuomba na kupewa
mistari ya kusoma now nikiomba nkimaliza tu nakuwa directed wap soma na nkisoma
ni kama napita mule mule. Nlishasahau kuomba kwa machoz jamani sa hivi ni kama
mvua et ,, sauti ya Mungu ilikua ndo kama nimesuswa jamani within hii time ni
kama rafiki ananisemesha sijui sa hata niseme nini, Dad nakupenda members
nawapenda Mungu atuimarishe.
GRACE
Namshukuru Mungu kwa maombi na
mafundisho kuna mambo ambayo nilikuwa nafanya kanisani nikaja nikaacha
nilipokuwa naanza maombi nikajiona jinga sana
ila leo nimeanza kufanya na ninaamini nitaendelea kufanya na zaidi,
Mungu akubariki dady tangu nimekufahamu sijajuta naamini Mungu atazidi
kukutumia na zaidi tutafaidi matunda mema aloweka kwako u zaidi ya mwl
zaidi zaidi ya baba hakika, Mungu
akutunze nimejifunza mengi kutoka kwako ubarikiwe wewe na familia yako kwa somo
la Repositioning nimemwona Mungu yaani kiasi ambacho sijawahi kabisa.
LAWRENCIA MASHIKU
Baba asante hata sasa sipo kama
nlivyokuwa ..nashukuru Mungu kwa ajili yako pastor Mungu akubariki...ushuhuda
wangu bado upo jikon....ila najiona watofauti saaaana.
MARIAM MWANTOGA
Namshukuru sn Mungu nimemuona kwa
namna nyingine kabisaaa.
Ni miaka kadhaa imepita tumekua
hatuna ibada ya pamoja na familia yangu, Mungu kanirejesha kwenye nafasi niliyo
ipoteza leo tumefanya ibada ya pamoja.
Mungu nakushukuru pokea sifa za
Moyo wangu, uinuliwe Bwana, pokea utukufu ee Mfalme.
Dady Raphael Mungu akuhuishe na
kukupa haja ya Moyo wako, akailinde familia yako kwaajili ya utukufu wake.
HOYCE FRANK
Nina mshukuru sana Mungu
nimejifunza nakujua mengi san nakujijua mimi nani nilikuwa nashiriki sana mambo
ya kanisa niliacha ile leo nimeenda na nitaendelea kwenda na nimejua nafasi
yang na nimejijua mimi nani asante sana pastor.
JANE MZIRAY
Kupitia maombi Haya Mungu
kanionyesha kitu cha ajabu Sana.
Kuna mtu alihamia katika eneo
ninalofanyia kazi na yeye akiwa mfanyakazi katika sector nyingine na akataka niwe rafiki yake. Sasa baada ya kuwa bad. Muda ukapta kuna
mambo flan flan akawa anayafanya na nilvyomshtukia nikakosa amani nae kabisa na
nikagundua vitu vingine ambavyo ni nje ya mapenzi ya Mungu... Sasa basi mimi
nikamueleza tu ukweli kwamba kutokana na mambo aliyo nayo siwez kuendelea na
urafiki uwe.... Kuanzia nilipomueleza hivyo nilibadilika sana nikawa mtu mwenye
hasira za ajabu nagombana na watu hadi wenzangu ofisini.. Nikiambiwa kitu
kidogo tu nakuwa mkali na mwenyewe hasira sana hadi nikawa najichukia
mwenyewe..
Jana nilvyokuwa kwenye maombi
Mungu kanionyesha kumbe huyo ndo chanzo
cha haya yote kwa hyo what I know niliingia kwenye maombi na kuikataa ile hali
na kuomba maombi ya ukombozi... Bado ninahitaji Hekima Ya Mungu ili niweze sasa
kutengeneza na wale ambao nimeshaharibu kwao. Kwa hiyo namshukuru sana Mungu kwa
hilo jaman..
ESTHER WILLIAM
Kwa kweli namshukuru sana Mungu
kupitia haya maombi, vilinyeyuka vita juu yangu,tangu ijumaa, kama
ningesikiliza mahubiri ya kipepo kwakweli nisingevuka ningebaki kama nilivyo.
Mungu ni mwema alinipa nguvu ya kutokutii vilivyo vikwazo vilivyojiinua,yaani
ninaamani sana moyoni baada ya haya maombi sasaivi nasikia ule uamsho ndani
yangu wa kuomba, ii hali ilikuwa imebalia ndani yangu neema tu ya Mungu,
nilifikia hatua ya kuomba mi mwenyewe naona kabisa haya maombi sijui kama Mungu
ameyasikia,yaani naona makavu. Ila sasaivi naomba huku naamini Mungu kayasikia,
Mungu pokea sifa na heshima kwa kutukumbuka watishi wako tuliokuwa tumetolewa
kwenye nafasi zetu, asante kwa kutulejesha Mfalme wa Amani tunakuinua Jehova.
QUEEN FLETCHER
Shalom famly,
Napenda kumshukuru sana huyu
Mungu kwa ajili ya program nzima ya repositioning fasting.
Well safari yangu ilianza hapa
kwa kusua sua lakini nimeimaliza kwa ushindi mkuu. Namshukuru Baba pia kwa
mafunzo yote na miongozo.Mungu akutunze.
Ni maombi yangu kila mmja
atayaishi na tuliyoyapanda na kuyaishi yote tuliyopata mahali hapa. Namshukuru
sana Mungu kwa ajili Ya upya huu ninaoufeeel sasa. Tuombeane wapendwa. Target
yetu kubwa n wote tukutane Mbinguni siku ile
Nawapenda .
Mungu awatunze wote.
Amen.
ESTHER MWAIJANDE
Wapendwa naomba na mimi niseme
kitu, before closet prayers nilipoteza kiu ya maombi na kusoma Neno. Nilikuwa
naomba kwa nguvu na kujikakamua sana lkn ukweli nilikuwa nilikuwa najua kabisa
kwamba hapa hamna kitu. Kila nikishika biblia nasoma mistari miwili naacha,
inaweza ikakata wiki sijashika kabisa bible. Nilikuwa najichukia sana but
kuchukua hatua nilishindwa coz sikujua nianzie wapi.
Baada ya kuingia Closet Players
tu siku ya kwanza moyo wangu ulipata amani na niliposoma notes za mafundisho
nilihisi mlainisho flani kwenye moyo wangu. Namshukuru Mungu amenirudisha
kwenye nafasi yangu, nikisoma Neno naelewa na kufunuliwa vitu kwa upana na kwa
kasi ya ajabu, nikiingia kuomba naomba kwa wepesi sana.
Ninamshukuru Mungu sana kwa ajili
ya ukombozi alioniletea kupitia mtumishi wake maana bila hivyo hali yangu
kiroho ingezidi kuwa mbaya sana. Mungu anisaidie na kunipa hekima ya kumantain hii nafasi. Mbarikiwe sana.
LORD I GLORIFY YOUR WONDERFUL
NAME.
Hakuna maoni: