DHAMBI NI MAARUFU KULIKO WEWE
Raphael, hata uwe nabii mkuu wa wakuu, au mtume aliyetumwa na anaetuma..askofu wa maaskofu...padri wa mapadri, kiranja wa mashemasi.....wewe bado ni mtu tu, wewe sio Yesu wala hutamfikia Yesu kwa lolote...ukiona watu wanaaanza kukunyenyekea na kukufanya kama JESUS ASSOCIATE APOSTLE(JAA)....unataka mtu anapokuja kukusalimia atambae kabisa eeee haha hahaha, Bwana Yesu alikuwa anakaa na wenye dhambi na wala hawatetemeki mpaka kutembea kwa magoti, ila wewe Raphael wewe Mungu akusaidie sana...
Unahangaikia nini kwani Raphael? STATUS QUO? Unataka heshima kwa kuwafanya wengine vibaraka wako? Hivi nani huwa anakuonya? Nani huwa anakukemea? Hata huyo anaekuonya hakuoni unavyoenda porini? Kweli wewe unaweza kuwa mkuu ndani ya mioyo ya watu kuliko KRISTO YESU? Unataka watu waombe kwa jina lako sio? Nini kinakusumbua mpaka unawalambisha watu mchanga na kuwalisha mbigiri kwa jina la maombi?
Nilikwambia kuwa kama vipi nenda kaombee maji ya ziwa Tanganyika ili iwe rahisi kuwahudumia watu wengi zaidi. NAKUKEMEA RAPHAEL. Unagombania nini kwani kama sio ubinafsi wako tu? Hivi Yesu angeweka haya mafensi yote nani angemsogelea? Nani leo anamzidi Yesu nguvu au umaarufu?
DHAMBI NI MAARUFU KULIKO WEWE ILA HAIJAWAHI KUBADILIKA KUWA KITU KINGINE.
HII POST NI YAKO WEWE RAPHAEL.
Hakuna maoni: