Ads Top

JISALIMISHE KWA YESU. GOD SUSTAINS



THE YARDSTICK OF TRUTH:

Kuamini huna akili au huna uwezo kwa kufeli mtihani wa masaa matatu au mawili ni ishara ya kujichukia inayomaanisha mawazo ya watu na waalimu yana nguvu zaidi kuliko uhalisia wa wewe ni nani. Uwezo wako hauwezi kupimwa kwa vyeti. DON’T LET PEOPLE’S OPINIONS MATTER TO YOU MORE THAN MATTER ITSELF. Mkubali Mungu ndani ya UFAHAMU wako nawe hutaishi tena chini ya kiwango. Watu wakikwambia huwezi, utakuwa na ujasiri wa kuwaambia anakupa nguvu ya kuweza sio maneno yao bali KRISTO YESU. Kumjua Mungu kunaleta afya ya akili na utulivu kamilifu wa moyo. Dhahabu hata uitupe kwenye matope haiwezi kugeuka kuwa matope. Inaweza kuchafuka ikiwa ndani ya matope, lakini haiwezi kupoteza UDHAHABU wake. Usipoteze thamani yako kwa kuwa tu kuna watu wanakuchafua na kukusema vibaya. Dhahabu ni dhahabu tu. Maoni na mawazo ya watu yaliyo kinyume na Mungu juu yakow ala hayana maana na wala yasikutaabishe. Ila lazima uamue kumkubali Mungu na unaweza kufanya hivo hata sasa. Tunawekwa huru kwa kuijua KWELI ya Neno la Mungu. JISALIMISHE KWA YESU. GOD SUSTAINS.

By Raphael JL:
0787110003

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.