Ads Top

KWA WAKRISTO WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA YA NETWORKING



KWA WAKRISTO WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA YA NETWORKING napenda kutoa ushauri binafsi usio na hila. Sisemi kuwa kufanya biashara hizi zinazoitwa NETWORKING,za kuongeza watu nyuma yako ili kupata fursa za kukua kifedha na kukua zaidi, sisemi kuwa ni mbaya. Ila ubaya unaweza kuwa ndani ya mtu kwa namna anavyofanya na uelewa wake kwenye hiyo NETWORK. Nimeona,wakristo wanaojishughulisha na biashara hizi ni watu VERY SOCIAL maana huo ndo mtaji wao,nimeona wengi wakiishia kuharibu mahusiano na wale waliowalenga kuwa ni wateja wao watarajiwa na hasa wanapokataa kujiunga. Nimeona mtu anakuja inbox kwa lugha nzuri, akionysha kukufahamu na kukuelewa sana, anakusalimia na ukishajibu tu anaanza kukwambia kuhusu hiyo biashara,akionyesha ni biashara nyepesi na inayoweza kukupatia kipato kwa njia rahisi sana. Ukikataa, ndo hamtawasiliana tena na hata anaweza kukupotezea hata kama alikuwa karibu na wewe. Sina shida na kwamba biashara hii ni sawa au si sawa. Nina shida na namna wakristo wanavyoharibu mahusiano na wenzao pindi mtu anapokataa kujiunga nyuma yake. Ninatoa angalizo tu kuwa NOT EVERYTHING THAT GLITTERS IS GOLD kwa namna ambayo mtu mwingine akikataa kujiunga unamuona kama Mpinga Kristo na hata kumchukulia kama mtu asiyetaka kufanikiwa kirahisi. Ni vizuri kujua kuwa pamoja na kwamba jambo unalofanya ni jema kwako,hii haimaanishi kuwa na wengine wanaona hivo na wanapokataa kujiunga basi huna haja ya kuwachunia na kuwaona hawafai tena kuwa rafiki zako. Tukumbuke pia kuwa watu wengine wana makovu ya biashara za kimtandao hapa Tanzania na nyingi ni majina tu yanabadilika lakini wazo kuu ni lile lile.Hivyo tunavyokuwa tunafanya hizi networking basi TUJIANGALIE NAFSI ZETU ili tusichafuke wala kuwachafua wengine kwa jambo ambalo ni maamuzi ya mtu binafsi. By Raphael JL:

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.