LADHA YA CHUMVI IKO NDANI YAKE, SIO NJE.
Point of Truth: LADHA YA CHUMVI IKO NDANI YAKE, SIO NJE.
Raphael, ujumbe huu wafikishie pia marafiki zako uwapendao na hasa maadui zako hata kama unaweza ukawa huwajui, wewe sambaza tu kwa kila mtu. Ni hivi, ladha ya chumvi haiku nje yake, ldha ya chumvi iko ndani yake. Mathayo 5:13, ninyi ni CHUMVI YA DUNIA; lakini CHUMVI ikiharibika itatiwa nini hata ikoleee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu. Raphael, umeelewa? Wewe ni chumvi ya dunia, fanya kazi ya chumvi na sio sukari. Wewe sio sukari ya dunia, wala sio sukari guru ya dunia na wala sio asali ya dunia. Wewe ni chumvi, na nataka nisemee jambo moja tu ndani ya chumvi au ndani yako ambalo naona kama vile siku zinavozidi kwenda kuna namna linapotea. Ladha. Ndio, moja kati ya sifa na kazi na maana ya chumvi ni kuleta ladha kwenye chakula, kwa maana ya moja kwa moja. Lakini Bwana Yesu hajasema wewe ni chumvi ya makande bali wewe ni chumvi ya dunia, yaani ndani ya maisha ya watu unatakiwa ulete ladha. Yaani watu wanatakiwa wakuelewe hivo, popote ulipo unatakiwa ulete ladha. Wewe ndo uwe wa kuigwa, yaani uwe mfano katika usemi, mwenendo, tabia, Imani na upendo. Kazi yako iwe na ladha, huduma, muziki, kitabu chako, kila unachofanya kinatakiwa kionyesha ladha ilofichwa ndani ya upekee wako na hasa baada ya kubadilishwa na injili ya Yesu Kristo. Maisha yako yanatakiwa yawavute wengi Zaidi kwa Yesu maana wewe ndio ladha, bila wewe kama chumvi chakula cha maisha ya watu wanaokuzunguka hakina ladha. Haya sasa.
Nimekufuatilia ile namna yako ya mambo unayofanya, sijui ujasiri umeupata wapi ila ngoja nikuulize hapa unambie. Nani aliyekwambia utumie mambo ya dunia hii ili kuwavuta watu wasioamini waamini? Je hujasoma kuwa INJILI NI UWEZA WA MUNGU UULETAO WOKOVU kwa Wrumi 1:16? Mambo yako mengine, na ya wale rafiki zako ni kama kwa sasa nashindwa kuwatofautisha kabisa na mambo ya dunia hii. Nawaangalia mnavyotenegenza mziki wenu na kuimba nyimbo zenu, jinsi mnavvyochanganya vionjo vya nyimbo za Extra Musica kwenye nyimbo zenu, mnavyochukua vionjo vya upigaji vya watu wasioamini mnachoamini na kusema kwa jina la Yesu mtavibailisha. Nimeona mnavyovaa, haha haha utanisamehe sana, nimeona mnavyotengeneza video zenu na closup zinazolenga kuonyesha makalio haha hahaha hahah aka UUMBAJI WA BWANA. Nimeona jinsi mnavyotafuta masomo ambayo mnasema hayawakwazi wengine, mnavyokataa kukemea dhambi na kukumbatia wenye fedha na kuwararua wasiojiweza. Naona kama mnaipenda dunia pamoja na mambo yake, au labda mimi sijui mambo ya dunia ni yapi, ona hapa 1 Yohana 3:9 inavyosema; kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi… ona pia hii hapa HUWEZI KUMPENDA MUNGU NA KUIPENDA DUNIA KWA PAMOJA, 1 Yohana 2:15, msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumoo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani tamaa ya mwili, na tamaa ya macho na kiburi cha uzima havitokani na Baba, bali vyatokana na dunai. Utofauti wako wewe Raphael na rafiki zako kinyume cha wasioamini wa duniani hapa ambao kumbe kwa ndani mnatamani mafanikio yao ni upi? Nini utofauti wake?
Unataka utende dhambi ili umfikie mwenye dhambi? Unataka usiamini ili umfikie asiye amini? Unataka uwe na disco ili uwavute vijana waendao disco? Unataka ufanye kama wao ili uwapate? Unataka utumie mbinu za mwilini kuwavua wa rohoni? Sijawaelewa bado. Nakazia hapa. Kumbuka, LADHA YA CHUMVI IKO NDANI YAKE NA SIO NJE. Nuru yanga’aa gizani, hivi bado inanga’aa? Mkiongea kama wao, mkila rushwa kama wao sema nyie mnakula kwa jina la Bwana, mkivaa kama wao, mkifanya yote kama wao ndo nuru inang’aa gizani? Kumbuka Bwana Yesu alikaa na wenye dhambi lakini hakutenda dhambi wala hakufanana nao bali wao walikuja kufanana na yeye. Hapo unahubirije kwa kupitia mwenendo wakati wao wakikusikia wanajiona ndani yako? Anyway. My point is LADHA YA CHUMVI IKO NDANI YAKE. Nakuja kumalizia hili punde.
By Raphael JL:
Instagram @ raphaellyela
Facebook page @Raphael JL:
Hakuna maoni: