NGUVU YA KUSIMAMA KATIKA NAFASI YAKO-1
NGUVU YA KUSIMAMA
KATIKA NAFASI YAKO
By Pastor Raphel JL.
TUMEUMBWA KUISHI ndani ya NAFASI ZETU, kila mmoja.
Usahihi wa kila kitu tunachofanya umebebwa na NAFASI tunayoitumia kufanyia chochote kile.
Ninaamini kuwa moja kati ya sababu kwa nini maombi yetu hayajibiwi kwa
wakati au hayajibiwi kabisa ni kuomba tukiwa NJE YA NAFASI ZETU.
NAFASI NI NINI?
Nafasi ni eneo ambalo mtu amepewa, au fursa au cheo ambapo mtu aliyepewa
anatakiwa kufanya mambo yake yote au KUISHI
MAISHA YAKE YOTE akiwa hapo. KILA
ANACHOFANYA LAZIMA KIFANYIKE TOKEA KWENYE NAFASI YAKE.
NAFASI imebeba KILA KITU.
NAFASI imebeba HATMA.
NAFASI imebeba KIBALI.
NAFASI imebeba KANUNI.
NAFASI imebeba FURSA.
NAFASI imebeba WATU NA RASLIMALI zote unazohitaji kufanikiwa.
NAFASI imebeba UPENYO.
NAFASI imebeba MAFANIKIO YA KWELI.
NAFASI imebeba MAJIBU SAHIHI.
NAFASI imebeba SILAHA.
Mwanzo 3:9
Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, uko wapi?
Tunaona katika Mwanzo 3:9,
Mungu anamuuliza Adamu, UKO WAPI-WHERE
ARE YOU?
Hili ni swali la NAFASI-POSITION.
Tungetegemea Adamu angeulizwa UMEFANYA
NINI.....lakini hakuulizwa hivyo, kwa sababu, UNACHOFANYA KIMEFUNGWA KWENYE NAFASI......
Kwa lugha ingine, Mungu anajaribu kuonesha hapo kuwa Adamu angekuwa
kwenye NAFASI YAKE asingekosea kwa
kumkubali mkewe kula tunda alilokatazwa. Kumbuka ADAMU HAKUDANGANYWA NA NYOKA BALI EVA. Aliyedanganywa ni Eva, ndiye
alianza kukosea lakini Mungu alipokuja hakuuliza EVA UKO WAPI kwani kila mtu ana nafasi yake. ADAMU NI KIONGOZI KATIKA UONGOZI, EVA NI KIONGOZI KATIKA USAIDIZI.
ADAM IS A LEADER IN A LEADING
ROLE AND EVE IS A LEADER IN A HELPING ROLE. THEY ARE ALL LEADERS BUT IN
DIFFERENT POSITIONS.
Eva asingekosea kama ANGESIMAMA
na KURIDHIKA na NAFASI YAKE ya kuwa MSAIDIZI
WA KUMFAA ADAM. Ila tunaona wote wawili walikosea. Eva alikosea kwa kuwa
alitoka NJE YA NAFASI YAKE. Na Adamu
alikosea pia kwa kutoka nje ya NAFASI
YAKE....How?
Eva alipofuatwa na nyoka alitoka kwenye nafasi yake kwa UJUAJI WAKE.
Adamu alitoka kwenye nafasi yake na akala tunda kwa HURUMA ZA KIMAPENZI KWA MKEWE.
Eva angebaki kwenye NAFASI yake
kama angemwambia nyoka, SIWEZI KUKUJIBU
MPAKA KIONGOZI WANGU AWEPO.
Adam asingekosea kama ANGEMSIMAMIA
VIZURI mkewe.
KILA MTU ALIKOSEA AKIWA NJE YA
NAFASI, lakini Mungu alipokuja akamuuliza KIONGOZI-MUME....UKO WAPI....Mungu hakuuliza “MKO WAPI?”
DIVORCE nyingi zinatokea
kwasababu kila mtu anakuwa NJE YA NAFASI
yake.....
Wanawake wanataka kuishi na kuwa kama wanaume. Wanaume wanataka kuishi
na kuwa kama wanawake.
MAHUSIANO MENGI YAMEKAA
KISHINDANI.
NDOA NYINGI ZIMEKAA KISHINDANI
KWANI KILA MTU ANATAKA KUFANYA AFANYALO NJE YA NAFASI ALIYOPEWA.
Kukaa na kuishi nje ya NAFASI ndio
msingi wa uharibifu wa mambo mengi sana mpaka leo.
UKO WAPI? Hili ni swali
gumu sana. Na ukisoma Biblia utaona watu hutoka kwenye nafasi zao kidogo
kidogo. Lakini sababu kubwa ni pale mtu anapofika na KUMKATAA MUNGU KATIKA FAHAMU
ZAKE. Yaani kutokukubali MAMLAKA
ya Mungu ifanye kazi ndani yake. Kutaka uhuru usio na mipaka.
Warumi 1:24-27
“Kwa aili ya hayo Mungu aliwaacha katika tama
za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao. Kwa maana
waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala
ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina.
Hivyo Mungu aliwaachia wafuate tama zao za aibu, hata wanawake
wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili; wanaume nao vivyo
hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tama, wanaume
wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki
yao.”
Unaona hapo WALIVUNJIANA
HESHIMA MIILI YAO.....maana yake walianza kuitumia miili yao kinyume na
namna iliyoumbwa na vile inavyotakiwa kutumika. KINYUME NA MAUMBILE. USHOGA NA USAGAJI.
Ukiwa kwenye mahusiano na kila kitu unataka kifanyike unavyotaka wewe
ujue wewe ni MSHINDANI na sio MKAMILISHAJI.....YOU
ARE THERE TO COMPETE, NOT TO COMPLETE.
NAFASI IMEBEBA USHAWISHI.
Kukaa nje ya nafasi zetu, ndio kinatufanya hata tunapoomba tunaomba
kama Mungu ni msela wetu mpaka wakati mwingine TUNAMFOKEA kabisa.
Mtoto anaejua nafasi yake kwa Baba yake, anapokuwa anaomba kitu huwa
anakuwaje vile?
Kutokujua nafasi zetu kumetufanya sisi tulio watoto wa mfalme tuishi
kama watumwa na watumwa wandunda tu kama watoto wa mfalme. ASANTE UJINGA.
Huwa tunatolewa nje ya nafasi zetu kwa NGUVU YA USHAWISHI inayochanganyika na kiwango fulani hivi cha
ujinga.
ITAENDELEA......
nzuri sana
JibuFuta