NGUVU YA KUSIMAMA KATIKA NAFASI YAKO-2
BY PASTOR RAPHAEL LYELA
...INAENDELEA (soma sehemu ya kwanza)
Ndio maana utaona watu wengi, hata mahusiano mengi huwa yanaharibika
zaidi kwa ushauri wa nje kutegemea ushauri huo unatoka wapi.
Mithali 1:10
“Mwanangu,
wenye dhambi wakikushawishi, wewe usikubali”
Kwenye eneo la ndoa, kwa mfano.....kinafasi, A MAN IS A LEADER. A WOMAN IS A HELPER.....kila mtu mwenye kutaka
kufurahia ndoa yake lazima aanzie hapo.....ni hatari kugombania nafasi ya mtu
mwingine.....
NAFASI IMEBEBA WAJIBU.
Wewe jiulize kama Adamu angewajibika. Kama Eva angewajibika. Au kama
wewe ungewajibika kwenye nafasi yako, mngepigana vibuti? Mngeachana?
NAFASI IMEBEBA UFAHAMU.
Mwanzo 3:9
Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, uko wapi?
Kuna mahali au kuna nafasi Mungu alimpa Adamu.....UKO WAPI.....ni kama Mungu anasema.....Adamu kuna nafasi nilikuweka
mbona sikuoni?
Kuna watu wanakuja kwenye maisha yetu ili TUWASAIDIE waweze kupiga hatua, ila kwakuwa huwa hatujui nafasi
zetu unakuta watu wanaishia kutongazana, kwa nini usipigwe kibuti? Mtu amekuja
ili awe mwanafunzi na mfuasi wako katika Bwana, wewe unaanza kuleta stori za mapenzi......laiti
kama tungejua.....ndo maana kuna watu unaweza hata usijue lini walipotea na
kuondoka karibu yako....kumbe ulianza kuongea pumba nje ya nafsi yako......
Kuna nafasi aliyonipa Mungu
kwenye mahusiano yangu na wewe.
Kuna nafasi natakiwa kumpa Mungu
ndani yangu.
Kuna nafasi yangu kwa mke
wangu.
Kuna nafasi yangu kwa watoto
wangu.
Kuna nafasi yangu kazini.
Kuna nafasi yangu kanisani.
Muheshimu mtu ambaye unajua amekupa nafasi ambayo neon lako moja
linaweza kuathiri maisha yake yote. JE
MUNGU SI ZAIDI?
Mwanzo 3:9...
9 BWANA Mungu
akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi?
Mungu alimuuliza
Adam...UKO WAPI? Ingawaje aliyekosea na kusababisha kosa ni Eva lakini Mungu
hakumuuliza Eva UKO WAPI.....tuendelee kidogo
NAFASI YA MUME
KAMA KIONGOZI HAIWEZI KUCHUKULIWA NA UJUAJI WA MSAIDIZI WAKE,BADO ATAWAJIBIKA
TU
Watu hutoka kwenye
nafasi zao zao kidogokidogo kwa ushawishi ujinga.
Mwanzo 3:10 inasemaje?
Mwanzo 3:10
Akasema, Nalisikia
sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha.
Utaona hapo kuwa
mtu ukiwa kwenye nafasi isiyo yako kuna mambo yanatokea...kwanza kila
utakachofanya utakosea hata kama kitawafaidisha wengine lakini pia HATA KUJIBU
UTAKOSEA.
Adam aliulizwa UKO
WAPI....akajibuje?
Ndo maana nimekuwa
nasema kuanzia mwanzoni kuwa hata maombi yetu mengi tunaweza tukaona HAYAJIBIWI
kumbe shida ni NAFASI tunayoiyumia kuomba hayo maombi.
Ni kama kusema
maombi pekee ambayo Mungu ameonyesha kuyasikia nakuyakubali na mtu akiwa nje ya
nafasi yake ni maombi ya TOBA,yaani maombi ya kugeuka.
Ukiona uko kwenye
mahusiano na unaona kila siku ni magomvi,yawezekana kabisa kuwa huenda mko kama
Adam na Eva...nje ya nafasi zenu...nje ya nafasi ni KUJILAUMU NA KULAUMIANA
TUUU
Ni kweli kuwa Adam
alimwambia Mungu kuwa ni huyo mwanamke aliempa...lakini je alikwepa LAANA?
Adamu aliulizwa
UKO WAPI....akakosea kujibu kwani alikuwa nje ya nafasi yake....Eva aliuzwaje?
Mwanzo 3:13 tusome.....
13 BWANA Mungu
akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka
alinidanganya, nikala.
Utaona hapo kuwa
Eva hakuulizwa UKO WAPI....aliulizwa UMEFANYA NINI kwani ile nafasi aliyofanyia
alichokifanya haikuwa yake ndo maana alikosea na lakini haikumfanya akose LAANA
na yeye. Kuitumie nafasi ya mwingine kukosea hakukufanyi wewe uwe salama.
So mke anapotoka
kwenye nafasi yake na kuanza kudai haki yake,ataishia kupigwa tu na mwisho hata
ndoa inaweza kuvunjwa...
Mume naye hivohivo
akitoka kwenye nafasi yake ya uongozi na kuanza kufanya anayofanya ataishia
kuleta ubabe tuuuu
ITAENDELEA....
ahsante sana
JibuFuta