NGUVU YA KUSIMAMA KATIKA NAFASI YAKO-4
...INAENDELEA
UTAJUAJE
KUWA UKO NJE YA NAFASI
DALILI
ZA MTU ALIYE NJE YA NAFASI YAKE
WARUMI 11:29
[29]Kwa sababu
karama za Mungu hazina majuto, wala mwito wake.
Yakobo 1:17
[17]Kila kutoa
kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba
wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka.
UKIONA HUNA AMANI
IPITAYO FAHAMU ZOTE-ujue umetoka kwenye nafasi yako
UKIONA MAJUTO NA
KUJIHUKUMU-Ujue umetoka
UKIONA HUNA FURAHA
YA BWANA-Ujue umetoka
UKIONA PIA KUWA
UMEANZA KUPOTEZA SHAUKU NA HAMU YA KUFANYA JAMBO,huenda ikawa kabisaa kuwa
umetoka
Ukiona umejaa
huzuni na malalamiko na masikitiko
Ukiona HUPATI
UTOSHELEVU
UKIONA ULICHOKUWA
UNAFANYA ZAMANI NI HERI KULIKO UNACHOFANYA SASA-huenda umetoka
Ukiona umejaa
kujitetea au kujiheabia sana haki...huenda umetoka
Kumbuka KARAMA AU
ZAWADI toka kwa Mungu HAZINA MAJUTO
Ukitoka kwenye
nafasi yako HATA MACHO YAKO YAANZA KUONA VIBAYA
Ukitoka kwenye
nafasi yako UZURI HUGEUKA UBAYA kwa haraka sana
Watu wameacha kazi
kisa, mishahara haitoshi...wakaenda kwenye mishahara mikubwa na kumuacha Mungu
kwenye mshahara mdogo-wanahangaika kama wafungwa na watumwa
Watu wameacha kazi
vijijini ili wawe mijini,wamemuacha mungu kijijini na wako mijini
wanahenya-kumbe mjini ni mungu pia...hatari sana
Ishu sio mshahara
mdogo...issue ni uko kwenye nafasi? Hakuna siku wafanyakazi wote duniani
watalipwa mishahara inayofanana. Au wote wakafanya kazi vijijini...ila
unapotaka kuhama au kubadilisha kazi, je umeomba ruhusa? Umeruhusiwa?
Uliomba kupata
kazi ukapata. Mbona unajiondokea?
Watu wanafukuzia
pesa, vyeo, kukaa mijini...wako tayari kufanya hayo yote hata bila mungu...watu
wanapenda kuteseka. Wengi wanafurahia.
Ukiwa kwenye
nafasi isiyo yako hata uelewa wako unabadilika
Tulia bana
Nilijifunza
kutulia
Nilipoanza kazi
nilikuwa na take home ya 470,000...niliona watu wakiacha kazi na kwenda kwenye
Malipo makubwa...MWISHO niliwaona wakirudi tena
Magomvi mengi sana
kwenye ndoa na mahusiano yangeisha kama kila mtu angesimama kwenye nafasi yake
Mwanaume akikaa
nafasi ya mwanamke anageuka kuwa kama dudu
Mwanamke akikaa
kwenye nafasi anageuka kuwa kama mganga wa jadi
Nimeona watu
wahama mikoa, kisa hawaipendi....wanaenda kwenye mikoa inayoonekana mizuri kama
kule alikoelekea Loti ambako ndo Sodoma ilikuwepo....Wanaacha mikoa ambayo wao
hawaipendi....wanamuacha na Mungu huko...wanaenda mikoa mizuri bila Mungu
Nimeona vijana
waliosoma kozi ambazo haziko kwenye nafasi zao chuoni...wanaishi maisha ya
kuchukia kazi zao maana hawakupenda tokea mwanzo ila waliambia KOZI HIYO INA
MKOPO....mwanasheria anaishia kuwa BANK TELLER
Unaweza kupewa
kazi inayoweza kukusaidia kukutoa kwenye nafasi yako....be very careful
sana....
Kuna watu utendaji
kazi wao unadolora toka walivyopewa promotion...promotion sio mbaya ila ikija
nje ya majira inaweza kuwa ishara kwamba unaenda kufukuzwa kazi hivi karibuni
Kuna viongozi
wanapobadilishiwa tu nafsi zao huanza kufanya vibaya kama vichaa
Kwanza IJUE NAFASI
YAKO...
Pili USHIRIKA NA
ROHO MTAKATIFU...LAZIMA UTAJUA TUUU
Wengine
wamechelewa kuoa na kuolewa kwani waliwaacha waume na wake zao kwenye maeneo
ambayo hawakuona kama mtu mzuri na sahihi anaweza kutokea huko...hata uende kwa
the greatest apostel of all time hakuna maombi ya kukupa mtu sahihi labda
maombi ya kulazimishia ambayo yatakugharimu milele....unakaa unajiona kama una
mkosi kumbe umejikosisha mwenyewe.
Ushirika na Roho Mtakatifu
ndio ufunguo wa kweli.
Kutokujua nafasi
yako kunaweza kukufanya ukubali hata offer za uharibifu.
Ni rahisi sana
kuoa na kuolewa na jiwe au nyoka kama uko nje ya nafasi yako.
Nje ya nafasi yako
utawasingizia watu hata kwa makosa yako mwenyewe
Kama huijui nafasi
yako, usiombe kurudishwa kwenye nafasi na huijui.
JE, WAIJUA NAFASI
YAKO?
KAMA HUIJUI BASI
IJUE
JE,UMETOKA KWENYE
NAFASI YAKO? BASI RUDI...sema tu kurudi lazima kuna gharama
MUNGU
AKUSIMAMISHE.
Ukijua NAFASI
YAKO,HUNA HAJA YA KUSHINDANA
ITAENDELEA...
Hakuna maoni: