Ads Top

PAMOJA KWA UMOJA


PAMOJA KWA UMOJA:THE UNPINGIKABLE POWER. YKM imekuwa inatumia neno Hilo kutoka Zaburi 133. Ni neno zito na Leo  tujifunze sehemu ya utajiri ulio ndani yake. Karibuni Sana. PAMOJA KWA UMOJA. IPO nguvu kubwa Sana ndani kuwa pamoja na kufanya mambo kwa umoja. Yapo makundi mengi ya Watu wanaojisema kuwa Wako pamoja na hata kauli za watu wengi wakisema TUKO PAMOJA. Ni muhimu kumalizia kwa UMOJA. Kumbuka wajenzi wa mnara wa babeli. Walikuwa PAMOJA na kwa UMOJA walifanya walichokusudia. Hawakuwa na unafiki. Hawakuwa waongo. Hawakuwa wabinafsi. Hawakuwa wavivu. Hawakujihesabia haki. Hawakukatishana tamaa. Hawakusengenyana. BALI. LAKINI. Walielewa kwanini wanafanya wanachokifanya na wakafanya kwa bidii. Walishiriki kwa PAMOJA na kwa UMOJA wao walimshusha Mungu. Katika uovu wa kuwaza kwao walikusudia kujenga mnara na walianza na MUNGU ilibidi aingilie Kati,Mwanzo 11:5.IPO nguvu katika kukusudia. Usikusudie bila kuelewa kwani BIDII KATIKA UJINGA NI KUJICHOSHA NA KUTAFUTA SABABU YA KUWAONA WENGINE WABAYA.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.