THE YARDSTICK OF TRUTH
The Yardstick of Truth: Raphael, Yohana 8:32 inasema hivi, tena mtaifahamu KWELI, nayo hiyo KWELI itawaweka huru. Halafu Yohana 8:36 inamalizia kusema, basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kwelikweli. Hapo hapo Raphael. Ninakuonya kwa upendo mkubwa kama bahari ya Hindi, uwe makini sana na watu ambao wanasema wanataka KUKUWEKA HURU kwa kupitia wanayosema ni KWELI lakini wakishakuweka huru wanakufunga kwenye MAMLAKA ZAO BINAFSI. Ukitaka kuoa wanataka uoe kwenye huduma zao, wamevunja mahusiano ya vijana tu kwasababu mtu hatokei kwenye kanisa lao na amegoma kubadilika kuwa kama wao. Nakuonya Raphael. Na wewe, usiwafanye vijana kama mali yako, kana kwamba una hati miliki yao, unawafuatilia kuliko upepo. Usiwanyang’anye uwezo wao wa kufanya maamuzi kwa kuwataka wakwambe kila kitu kwenye maisha yao, usimzidi Mungu ambae alitoa utashi bila kuingilia maamuzi yetu.
Nakuangalia sana unavyoenda, Yesu anakufundisha nini? USIWAFUNGE ALIOWAFUNGUA kwa kuwabana hata wasiende kwenye semina za watu wengine kisa unajiona wewe ndo una mafundisho sahihi dunia nzima. Angalia sana Raphael. Watu ni wa Mungu. Vijana ni wa Mungu. Wewe ni WAKILI WA SIRI ZAKE. Usinyenyue pembe kuliko uwezavyo. Usiwafanye vijana wakuone wewe ni ALFA NA OMEGA, like una majibu ya kila kitu, unajua kila kitu as if wewe sio mwanadamu mwenye mapungufu ambayo huenda yangefunuliwa kwa wengine ungekuwa mdogo kama piritoni. Nielewe nisemacho, nakwambia wewe Raphael kwani wewe tu ndo unanielewa vizuri na pia nakwambai haya kwa upendo na sio majungu wala hila. Usiwafunge wale ambao Bwana Yesu amewaweka huru tayari na wamekuwa huru kweli kweli. Uhuru wa aliye huru usiuchanganye na ubinafsi wako wa kutaka ukuu na kunyenyekewa kama mfalme.
By Raphael JL:
Instagram @raphaellyela
Hakuna maoni: