Ads Top

UBAYA WA UBINAFSI, UZURI MBAYA ULIOFICHWA NDANI YA NAFSI



Raphael JL:
4.04.2017
UBAYA WA UBINAFSI, UZURI MBAYA ULIOFICHWA NDANI YA NAFSI

Inauma sana. Inaboa na kwakweli inakatisha tamaa sana. Wewe fikiria uko kwenye group la whatsapp au telegram au uko wenye FB au INSTA au tu uko kwenye kundi la watu zaidi ya mmoja. Wewe unapost jambo lako ukitegemea watu watalifurahia au watachangia. Ila unaona kimyaaaa, halafu hapo hapo mtu mwingine anapest kichekesho, unaona watu wanavyochangamkia. Unaleta shida yako na unapost lakini watu unaona kabisa wamesoma ila ndo hivo penye miti hapana wajenzi. Kila ukijitahidi, hata unaanza ujifanya una jambo ili watu waje ndo useme, uaona tu mtu ametuma EMOJI lakini kimya.

Kabla hujawalaumu sana, unatakiwa ujiulize kama hivyo sivyo hata wewe unawafanyia wengine. Huwa huchagii mpaka umeguswa ujue watu hawatachangia mambo yako mpaka wameguswa. Kanuni ni ile ile, usiposhiriki mambo ya wengine na wewe jiandae kufanya jambo lako na upepo. Usichotaka kufanyiwa usiwafanyie wengine. Usichotaka kutendewam usiwatendee wengine. Usichotaka kuambiwa, usiwaambie wengine. Usikotaka kwenda, usiwapeleke wengine. Usichotaka kuvaa, usiwavishe wengine. Usichotaka kula, usiwalishe wengine. Hii ni kanuni ya dhahabu aliyoisema Bwana Yesu.

Unataka kupendwa, basi penda. Unataka watu wachangie post yako basi na wewe changia za wengine. Unataka watu wakukumbuke, na wewe usiwasahau. Unataka kusaidiwa, basi anza kwa kusaidia. Kuwepo kwenye group ambalo hufanyi chochote na wala huchangii chochote ni usaliti wa ajabu sana. Na heshim huonekana wakati una shida yako. Unataka watu wakupigie kura ili ushinde tuzo Fulani na huku wewe huwa husambazi jumbe za wenzako wanapokutumia wala huwa hujitoi kwa mambo yaw engine ujue kazi unayo. Huu ndio ukweli. Kama unabisha, wewe subiria utakapoanza kutaka kuoa au kuolewa, au utakapopatwa na shida ambayo inahitaji watu. Jifunze kuishi na watu. SHIRIKI MAMBO YA WATU,WATU WATASHIRI MAMBO YAKO. Maamuzi ni yako.


By Raphael JL@April 2017.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.