UKWELI
Point of Truth: Raphael, ukiambiwa ukweli wa maisha yako usimchukie anaekwambia kwani ni kwa faida yako. Ni heri mtu anaekwambia ukweli kweupe kuliko anaekuchekea, wengi huwa wanajipendekeza. Nakushauri kweupe kila siku ili na wewe siku moja usije ukaanza kuuza maombi kwenye bahasha, ili usije ukakaharibu moyo wako kwa kuanza kula kondoo unaowalea, ili usije ukaanza kuyauza maji yaliyoombewa wakati una uwezo wa kuombea maji yote ya Ziwa Tanganyika ili watu wawe wanachota tu, ili kwamba usije ukataka kuheshimiwa heshima ya kuabudiwa kwani unataka hata mtu anapokufuata akupigie magogi akitambaa mbele zako. Huu ni ujinga Raphael na sitaacha kukukemea. Hata Yesu mwenyewe ambae wewe unamtumikia wewe leo hakuwa hivo, sijui matabia mengine ya kipuuzi haya umejifunzia wapi. Angalia sana. Nakukemea Raphael.
By Raphael JL:
Instagram @raphaellyela
Hakuna maoni: