Ads Top

UNAIPENDA NJIA, MTU AU HATMA



RAPHAEL, UNAIPENDA NJIA, MTU AU HATMA
Kuna mtu alishawahi kukuomba kwamba anataka kuambatana na wewe? Au kuna mtu ulishawahi kumwambia aje aambatane na wewe? Hayo mawili hayafanani kijana wangu Raphael. Utofauti wake ni huu, mwanzilishi wa Jambo ana sababu kubwa ziadi nyuma yake. Anaeona unaenda na anataka kukufuata ana sababu kubwa moyoni mwake. Leo nilikuwa natafakari, unaweza kupenda kutembea na mtu kuelekea mahali fulani kuliko unavyoipenda njia yenyewe n ahata kuliko unavyopenda kufika mwisho wake. Hapo msisitizo uko kwenye MTU. Ila unaweza kuipenda njia Zaidi kuliko mtu unaetembea nae wala kule unakoenda. Hapo msisitizo ni NJIA. Na unaweza kupenda kule unakokwenda kuliko uko na nani na unatembea juu ya njia gani. Hapo msisitizo ni HATMA. Jiulize hapo ulipo, katika hayo matatu wewe uko kundi gani?

Halafu Bwana Yesu anasema, yeye ni NJIA, KWELI na UZIMA. Yesu ni yote hayo matatu.

By Raphael JL:

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.