Ads Top

USHUHUDA WA DADA CELINA KUTOKA MAOMBI YA MASAA 36 (CLOSET PRAYERS)





USHUHUDA WANGU 

Utangulizi:-

Mnamo Tarehe 10/08/2017 nilijiunga rasmi ndani ya hii Safina. Kupitia rafiki yangu mpenzi Mrs Amina Myombo. 

Nikajitambulisha hivi:-
Mrs Celina Magigita. Nimeokoka, mfanyabiashara, kihuduma ni mwalimu na mhubiri, ninaishi Dodoma. Nipo humu kwa nia ya kuvuka nilipokwama. Asanteni kwa ushirikiano. Nimesoma masomo kupitia dada Amina,  nimebarikiwa sana. Tupo pamoja ndugu katika Kristo Yesu.

Shauku na Nia yangu kuu kujiunga humu ilikuwa KUVUKA NILIPOKWAMA!. 

Neno linasema:-
"Nawe utakusudia neno, nalo litathibitika kwako; Na mwanga utaziangazia njia zako". (Ayubu 22 :28)

Kusudi langu halikuwa kuja kufahamiana na watu au kushangaa bali nilikusudia KUVUKA. nilimaanisha nilichokusudia na nikadhamiria KUVUKA. 

Leo hii ikiwa siku 10 ndani ya SAFINA ninazo shuhuda kuu 3 za matendo makuu ya Mungu naam na ya 4 iko njiani naitarajia kuipokea wakati wowote ambayo ndiyo muhimu zaidi kwangu. 

Mambo niliyotendewa ni:-

1. Akili zangu zimefunguliwa nimeelewa ili kuishi maisha ya Ushindi jambo kuu ni kuwa na UFAHAMU sahihi wa hilo eneo. Kwa hiyo nimejipanga kulipa gharama kujaza moyo wangu maarifa ya kiungu ili nipate ufahamu wa kutosha kuishi maisha ya utoshelevu na ushindi huku nikilitumikia shauri la Bwana. 

2. Asante Ujinga imeniondoka, nimetembea kwenye mateso ya kujitakia ndani ya ndoa yangu kwa zaidi ya miaka 17. Kupitia maarifa niliyoyapata humu nimeweza kufanya maamuzi magumu ya kukaa kikao cha masaa 3 na kuwekana sawa na mume wangu hatimaye tumerejea Eden. Hali haikuwa nzuri kama ni shimo basi adui alishaliweka tayari kunitumbukiza. Asante mchg. Raphael kwa kunivusha nisitumbukie. 

3. Eneo la uchumi limekuwa na mapito mengi sana na sintofahamu za hapa na pale. Kwa neno la mwisho alilonipa Bwana kwa njia ya ndoto nilipokuwa nahitimisha maombi. Limetosha kunipa kujua BWANA ananirejeshea utukufu wa NAFASI yangu kiuchumi. 

4. Eneo la Kiroho hili ni nyeti zaidi kwangu na sijaelewa kwa nini Mungu amelifanya kuwa la mwisho kukamilishwa muujiza wake! 

Nimekuwa katika mapito magumu sana yaliyopelekea mahangaiko ya kutokuwa na mchungaji mmoja wa kunilea kiroho kwa muda mrefu na shida kubwa ilikuwa baba wa familia kutaka nibaki kwenye dini nami nang'ang'ana kutaka kumtafuta Mungu kiroho zaidi badala ya kujifungia kwenye kifungo cha dini na mapokeo ya dhehebu. 

Juzi kwenye toba na matengenezo nilikaa na mume wangu nikafanikiwa kujieleza kwa msaada wa Roho Mtakatifu hatimaye amenielewa na kukubaliana na ombi langu la mimi kupewa uhuru wa mahali pa kuabudu kiroho.

Huu kwangu ni muujiza mkubwa sana lakini haujakamilika bado ndio kwanza nimeanza kuomba Mungu anipe mchungaji sahihi wa kunilea kiroho ikiwa ni pamoja na huduma na utumishi uliomo ndani yangu.

Bwana ameahidi,
"nami nitawapa ninyi wachungaji wanipendezao moyo wangu, watakaowalisha kwa maarifa na fahamu" (Yeremia 3 :15)

Suala si kuwa ndani ya kanisa maarufu, jengo zuri nk.... Muhimu kwangu ni ninalishwa nini na hicho ninacholishwa kinanipa maarifa na ufahamu wa kutosha kuishi maisha ya utoshelevu pande zote na yanayompendeza Mungu! 

Kwa huyu mtoto wa 4 ni muujiza ambao haujakamilika nawiwa kusema haya kwa pst Raphael. 

Petro alitekewa alipokuwa uweponi mwa Bwana akaishia kusema na tujenge vibanda vitatu.. ...nahisi kuna mambo aliona bado hayajapatiwa majibu akatamani waendelee kubaki mahali pale kwa muda zaidi ili apokee yote kwa ukamilifu wote. 

OMBI LANGU. 

Humu ndani sijui kama wote tumevuka kwa kuzaa vile tulivyoingia nanvyo ndani ya Safina na tumetosheka kwa vile tulivyofanikiwa kupush hata tukazaa. 

Binafsi mtoto namba 4 hajazaliwa mkamilifu ni premature anahitaji kusaidiwa ili akamilika na leo ndio mwisho wa hii incubator nawaza peke yangu joto nililo nalo litatoshea kumkamilisha! Bado sijaliamini joto langu hivyo ninaomba extension ya muda atakaona unafaa mbeba maono pst Raphael ili mtoto huyu akamilishwe na kukamilisha ushuhuda huu muhimu kwangu kiroho. 

Naomba hekima yako mtu wa Mungu na muongozo ikiwa nitapata kibali moyoni kwako. 

Jambo moja ninajua hakuna mtu anayefanikiwa pasipo msaada wa watu wengine. Kwa hilo nilijifunza nimejifunza  kunyenyekea na kuheshimu mchango wa watu kwenye hatma yangu. 

Mchg. Raphael umeongeza thamani yangu kwa kuniweka kwenye njia sahihi kuielekea hatma yangu ya utukufu. Ni maombi yangu Mungu akuinulie watu wakuu watakaokushika mkono na kuongeza thamani ya maisha yako hata uufikie ukamilifu wa hatma yako duniani. 

Nawapenda katika wote Bwana. Mmefanyika baraka kwangu kwa hizi siku 10, niliomba ushirikiano nilipoingia humu, namshukuru sana Mungu kwa ajili yenu kwani mmenipa ushirikiano mkubwa na kunirahisishia kupokea kwa kasi ya ajabu. 

Barikiweni,
Celina


Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.