USIKATE TAMAA
TRUTH POINT:
Usikate tamaa. Usirudi nyuma. Usiache unachofanya. Usishushe viwango. Usiyumbe wala kuyumbishwa. Kama unachokifanya ni sahihi. Kama unachokifanya ni sawa. Kama unachokifanya unakiamini. Unajua ngoja nikwambia, hakuna jambo rahisi au jepesi ambalo lina harufu ya mafanikio. Mungu akikupa jamb na kukuwekea shauku ya kulifanya basi uwe na hakika kuwa litapigwa vita, litazuiwa na kupingwa njia moja au nyingine. Usiogope na kukata tamaa.
Kama unamwamini Mungu huna sababu ya kukata tamaa, kama una Imani kwa Mungu usikubali kurudi nyuma. Nakuandikia leo kwamba USIKATE TAMAA. Adui atakucheka sana. Atakuzomea. Simama imara mwana wa Mungu. Hata kama umeomba kazi na kufanyiwa usahili mara 12 kumbuka kuna mara ya 13 pia. Hata kama umejaribu kukaa kwenye mahusiano lakini yanavunjika pale yanaponoga, MSIKILIZE MUNGU, hakuna kitu Mungu hajui, atakusaidia. Usizitegemee akili zako.
Unataka kuacha kufanya biashara yako eti kisa umepata hasara sana, acha utani, huwezi kupata hasara kama hasara ya kukubali kushindwa. Umeacha kuomba juu ya uhamisho kisa haijaruhusiwa, we omba tu zitaruhusiwa chache na yako imo. Umeacha kuombea mtoto, kisa historia inaonyesha umejaribu mara 7 na imegoma, sawa kuna mara ya 8 halafu kumbuka ANAEZALISHA NI MUNGU, anajua mahesabu yote. Amini. Mwamini Mungu. Hujachoka kwa kiwango cha kukosea au kukata tamaa.
Neno langu kwangu kwako ni hili, Luka 1:37…KWA MUNGU, YOTE YANAWEZEKANA. HATA LAKO LINAWEZEKANA.
By Pastor Raphael JL: @0787110003.
Amen, asante kwa somo zuri
JibuFuta