USILAZIMISHE, YAWEZEKANA MUNGU ANAKUSEMESHA
USILAZIMISHE, YAWEZEKANA MUNGU ANAKUSEMESHA
Umefanya mara kwanza ikagoma. Umefanya tena bado ukafeli. Ukajaribu na kufanya tena ikafeli. Kila mdada ukimfuata anakukataa. Kila mkaka akikufuata anataka ukae nae kwa kufanya dhambi. Umejaribu kila biashara inagoma. Siku unataka kusafiri unachelewa gari. Kazini ni kama inaonekana unakaribia kufukuzwa au kufanyiwa zengwe. Watu wanaokuzunguka hawakuelewi, ni kama kila mtu anakushangaa vile ulivyo sasa. Huioni Amani na furaha uliyodhani ungekuwa nayo kama ungepata ulichonacho. Ni kama watu awakuelewi kabisaa. Wewe mwenyewe ukijiangalia hata kwenye kioo hujielewi. Watu hawataki kukaa karibu na wewe na ukijikaribisha ni kama hakuna anaekushangilia. Shule umefeli. Kazi hupati. Biashara haziendi. Mume hakuelewi. Mke hakuelewi. Watoto hawakuelewi. Unahisi hata upepo haukuelewi.
Unajaribu kufanya unachofanya ila ladha ya kufanya inapotea na shauku inaondoka. Unapita njia fulani ghafla unajisikia kukosa Amani. Unakutana na mtu unajitahidi kumchangamkia ila ndani yako unaona kama sio vile. Unataka kuacha kazi ila ndani yako unaona kama unakosea vile. Unataka kuhama kazi lakini ndani yako huna Amani.
USILAZIMISHE,YAWEZEKANA MUNGU ANAKUSEMESHA.
Wengi tumekosea sana hali hizo zikitutokea. Tumekuwa hatujui maana yake wala hatujui kutafsiri hizo hali. Huenda zimesababishwa na dhambi au sababu yoyote ile ila kwa leo mimi nataka tu kusema kuwa ukiona hali kama hizo usilazimishe, huenda Mungu anakusemesha kwa njia hiyo maana labda alikusemesha hukuelewa. Ulimwengu wa leo watu tuko busy sana kiasi kwamba kumsikia Mungu anaezungumza tokea ndani kwa Roho Mtakatifu inakuwa ngumu sana. Kwahiyo tunajikuta tuna majuto mengi sana. Tunajilaumu sana kwa kuamua vile. Kwanini hatukuamua hivi. Mpaka wakati mwingine tunafika mahali ambapo hatuelewi tena kipi ni sawa na kipi si sawa. Ninachosema ni rahisi sana, hali kama nilizotaja hapo juu zinapotokea watu hulazimisha n ahata kujipa maana zao na kujikuta wamekosea zaidi. Wengine hukata tamaa na hata kuacha walichokuwa wanafanya. Wengine huamua liwalo na liwe.
Ushauri wangu ni rahisi sana. Ukiona hali kama hizo, ukiona mazingira kama hayo usilazimishe kusukuma hilo jambo. Huenda hiyo hali ni ishara tu na lugha ya kukwambia kuwa unakosea au hutakiwi hapo au kaa chini jifanyie tathmini ya kimkakati. Kubwa kuliko yote ni kumuuliza Mungu juu ya hiyo hali maana Mungu anajua kila hali tunayopitia. Na ili hili liwe na nguvu basi ni lazima kuwa na UTII WA HALI YA JUU kwani mtu anapopita kwenye hali kama hizo huwa anakuwa kama hajitambua na unaweza kuamua lolote. Kama leo ulitaka kuamua lolote basi nakushauri, usilazimishe, yawezekana Mungu anakusemesha.
Yaani kuna watu wako busy mpaka kama unataka kuongea nae ni lazima aumwe ndo utampata. Huenda kuna watu wanaumwa, unapima vipimo vyote na huoni kitu, kumbe umeumwa tu ili ulazimishwe kupumzika maana uko busy sana. Yawezekana. Ila ninalosema ni hilo tu, yawezekana kwamba hali unayopitia ni ishara na dalili. Huenda unapewa tahadhari kuwa kuna kitu kinakuja. Ni vema sana ukiwa unapita kwenye kipindi kama hicho kujiuliza na kutaka kujua mawazo na ushauri wa Mungu juu ya jambo hilo. Badala ya kuanza kulalamika na kulaumu na kujikosesha raha na amani.
OBIDIENCE IS NOT GIVEN. OBIDIENCE IS EARNED.
By Raphael JL:@0787110003
Nmejifunza kitu Asante Mwalimu
JibuFuta