USIVIANGALIE VINAVYOONEKANA
Raphael, 2 Wakorintho 4 : 18 inasema hivi tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele. Liweke hili neno moyoni mwako na leo unapokunywa chai lihanganye hili neno ndani ya kikombe cha chai na mchana ulifanye kama pilipili kwenye chakula chako. Naongea na wewe Raphael mtu wa Mungu, USIVIANGALIE VINAVYOONEKANA kwani ni maamuzi yako kuamua kuangalia nini. Huu ni ushauri wa kiMungu tu kwako. Vinavyoonekana vina udanganyifu mkubwa sana. Vinavyoonekana vina tabia ya kulazimisha maamuzi ya haraka kwani vinashika sana hisia zetu. Vinavyoonekana vina tabia ya kulazimisha tamaa mbaya na mpaka unaweza kujikuta UNALEGEZA VIWANGO na kujikuta unaiba, unakula rushwa, unasema uongo, unafanya uasherati na uzinzi. Nakushauri leo siku ya kwanza ya mwezi wa tatu 2017.
Kwamba vinavyoonekana ni vya muda tu. Yaani havidumu na vinaharibika. Ndo maana siku ileee nilikushauri ujifunze kuweka HAZINA YAKO MBINGUNI kwani huko ndio hazina ya kweli inaweza kudumu. Kwakuwa vinavyoonekana ni vya muda mfupi basi moyo wako usibebwe navyo wala usiharibu utu wako kwa hivyo kwani ni vya muda mfupi na vinapita. Ila ni vizuri ujiulize, nisije nikadhani unaelewa na kumbe huelewi ninachosema. JE, UNAVIJUA VINAVYOONEKANA NI VIPI? JE, UNAVIJUA VISIVYOONEKANA NI VIPI?
By Raphael JL;
Hakuna maoni: